Mtuhumiwa wa kesi ya ubakaji dhidi ya watoto mwalimu Andrea Shedrack akitoka mahakamani kutoa ushahidi wake katika mahakama ya hakimu mfawidhi mbarali mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbarali
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbarali, imefunga ushahidi wa
upande wa utetezi katika kesi ya kubaka wanafunzi watatu wakike wa Shule ya
Montford High School ya Rujewa kwa nyakati tofauti inayomkabili aliyekuwa
Mwalimu wa shule hiyo Andrea Shadrack.
Mshtakiwa huyo akifunga ushahidi wake ameiambia mahakama
hiyo kutupilia mbali mashitaka dhidi yake kwakuwa ni ya uongo.
Hayo yalidaiwa mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi, Kinabo
Minja, baada ya mwendesha mashitaka wa polisi Meja, Mazoya Luchagula
kufunga ushihidi wake dhidi ya mshitakiwa huyo.
Awali kabla kesi hiyo haijafungwa upande wa mashitaka
ulileta mashahidi wake watatu ambao ni wanafunzi wa shule hiyo ambao waliiambia
mahakama jinsi mwalimu huyo alivyokuwa akiwarubuni na kuwaingilia kimwili.
Mashahidi hao waliimbia mahakama kuwa Mwalimu
huyo aliwafanyia kitendo hicho September
12, mwaka 2013 majira ya saa 3:30 usiku huku mwanafunzi wa
pili alifanyiwa siku hiyo hiyo majira ya saa 4:00 usik.
Ushahidi
huo uliendelea kuweka bayana ya kwamba katika tukio la tatu Mwalimu huyo
inasemekana alimwita mwanafunzi huyo kutoka bwenini na kisha kumbaka huku
akimlaghai ya kwamba licha ya yeye kupata uhamisho lakini atarejea
shuleni hapo na kuwa Mkuu wa Shule.
Hata
hivyo Akifunga ushahidi huo, Hakimu Kinabo alisema mahakama imemaliza
kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kutaja tarehe ya hukumu ambayo
itatolewa Mei 14 mwaka huu.
Mwisho.
Post a Comment