Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Nouman Sigalla akizungumza katika semina ya Afya ya Msingi iliyo fanyika katika Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Mbeya. |
Mganga Mkuu wa Jiji la Mbeya Daktari Samwel Lazaro akifafanua jambo katika semina hiyo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Wataalam wa Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na
Jiji kwa ujumla watakiwa kuwa makini
katika utaoaji wa Chanjo ya surua na polio kwa watoto wenye umri miezi 24 na 18
.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Mkuu wa Wilaya ya
Mbeya Daktari Nouman Sigalla wakati akifunga semina ya Afya ya Msingi ambayo pia imejadili taarifa za utoaji wa chanjo ya pili
itakayo anza kutolewa mwanzoni mwa mwezi
mei mwaka huu.
Amesema kimsingi kumekuwepo na udhaifu katika utoaji wa
chanjo ya kwanza hasa kutokana na kuwepo kwa madhara yatokanayo na chanjo hizo
mara baada ya kutolewa kwa wahusika.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hatua ya utoaji wa chanjo ya
pili ya surua inatokana na kuwepo kwa
madhara yanayojitokeza mara baada ya kupatiwa chanjo hasa kwa kuhusisha maradhi
mbalimbali pamoja na ugonjwa huo wa sura
kuibuka upya.
Amesema kiini cha tatizo hilo ni kutokuwepo kwa umakini wakati
kwa watoa huduma hiyo kwa kushindwa kufuata masharti pamoja na
kushindwa kuwafikia watoto wote wanaopaswa kupewa chanjo hiyo.
Dokta
Sigalla amesema nivema sasa wataalamu hao wakawa waangalifu katika
uchanjaji huo pamoja na kufuata masharti yake .
Kutokana na hali hiyo amewataka maafisa watendaji ,maafisa
ugani pamoja na vijiji mtaa na tarafa kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya kuhamasisha wananchi kupeleka watoto kupata
chanjo hiyo
Amesema pamoja na uhamasishaji huo kwa wananchi hao nivema pia wakapita nyumba hadi
nyumba kwa lengo la kupata taarifa sahihi juu ya wale wanao takiwa kupata
chanjo hiyo ili kufikia lengo husika.
Amesema nivema kila mwisho wa mwezi zikatolewa taarifa kwa
halimashauri juu idadi ya watu waliopata chanjo hiyo ili kupata taaifa sahihi
zitakazo saidia kupunguza au kuondokana kabisa na tatizo hilo.
Akizungumza suala la utoaji wa chanjo hiyo ya pili ya
surua Mganga Mkuu wa jiji la Mbeya Daktari Samwel Lazaro amesema kuwa maandalizi
yake yamekwisha kamilika kwa
kiwango kikibwa kwa ajili ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.
Aidha, amesema dhamira ya chanjo
hizo ni kuwakinga watoto na maradhi mbalimbali yanayoweza kuzuilika kwa chanjo
ikiwemo polio, pepo punda surua na mengineyo.
Amesema lengo kuu la chanjo hiyo ni
kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2020 tatizo la maradhi ya watoto
yanamalizwa au kupunguzwa kwa asilimia kubwa.
Amesema kazi hiyo itaanza katika vituo vyote vya afya kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku zote saba.
Semina hiyo imehusisha wataalam wa afya viongozi wa dini
pamoja na wadau mbalimbali wa afya kutoka maeneo mbalimbali katika halmashauri
hizo
Mwisho.
Post a Comment