Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi


Na EmanuelMadafa,Mbeya

Hatimaye Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama barabarani  Wilaya za Rungwe na Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.

Askari hao ni pamoja na  Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo ambao walikuwa wanafanya kazi barabara ya Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.

Wengine ni   Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon ambao walikuwa wakifanya kazi katika eneo la Songwe katika barabara ya Mbeya Tunduma.


Akizungumza hali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Ahmedi msangi amesema Askari hao walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa adhabu ya kufukuzwa kazi.

Hata hivyo msangi amebainisha kuwa Askari wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha,WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.

Amesema Wengine wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ni DC Marcelino Venance mwenye namba 8084,PC Juma Idd mwenye namba 3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson Mwakalobo ambao walidaiwa

Aidha Kamanda Msangi amesema Jeshi lake halitasita kuwafukuza kazi Askari watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi na Askari yeyote atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.
mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top