Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi


Na EmanuelMadafa,Mbeya

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ikifuatiwa  Chunya zimetajwa kuongoza katika vitendo vya ubakaji kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

Kwa Mujibu wa  Taarifa za Mwezi zilizotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani mbeya ambazo zinaelezea tathimini ya makosa mbalimbali kwa mkoa wa mbeya zimedai kuwa makosa ya  ubakaji na ulawiti Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imekuwa kinara zaidi ya Halmashauri nyingine za mkoa huo.

Aidha kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya pekee ina jumla ya makosa ya ubakaji na ulawiti ni 66 ikifatiwa na Chunya yenye makosa 21ambayo ni ubakaji  tu

Pia maeneo mengine yanayo fuatia kwa vitendo hivyo ni pamoja na Mbarali na Rungwe  kwa kuwa na makosa 16.


Pamoja na kuwepo kwa vitendo hivyo vya ubakaji  taarifa hiyo imebainisha kuwa katika Katika kipindi hicho cha Jan – Machi, 2014 jumla ya makosa ya jinai  6,473 yaliripotiwa, wakati kipindi kama hicho mwezi Jan – Machi, 2013 makosa 6,853 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 380 sawa na asilimia 6.

Hata bhivyo Katika kipindi hicho cha Jan – Machi, 2014 jumla ya makosa makubwa 594 yaliripotiwa, wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013 makosa 601 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 7  sawa na asilimia 1


Mwisho.





Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top