Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
 Na EmanuelMadafa,Mbeya
Wekundu wa Msimbazi Simba Spots  Club ya jijini Dar es Salaam yadaiwa kuchukua wachezaji wawili machachari toka club ya Mbeya  City Fc ya jijini Mbeya.

Wachezaji wanaodaiwa kuchukuliwa na Wekundu hao ni pamoja na Saad Kipanga na Deus Kaseke ambao wanatajwa kuwa tegemezi kubwa kwa Timu hiyo ya Mbeya City .

Kwa mujibu Chanzo Chetu cha habari  kimedai  kuwa teyari mazungumzo baina ya wachezaji  hao wa Mbeya City na uongozi wa Simba yamekwisha fanyika ambapo kwa sasa yapo katika   hatua nzuri.

Chanzo hicho kimedai kuwa mazungumzo ya wachezaji hao yalianza mara baada ya kukamilika kwa mchezo wa Tanzania Prisons na Rhino Rangers ya mjini Tabora  uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini hapa.

Amesema mazungumzo hayo yalikuwa kati ya wachezaji hao pamoja na baadhi ya viongozi na kocha mkuu wa Simba .

Pia Chanzo hakikuweka bayana juu ya mkataba huo kuwa ni wa  muda gani pamoja na mishahara watakayolipwa wachezaji hao licha ya kudai kuwa ni mshahara mnono totauti na walichokuwa wakilipwa awali na Mbeya City.
Deus Kaseke pichani
Kufuatia hali hiyo blog hii imepata fursa ya kuzungumza na uongozi wa mbeya city juu ya kuwepo kwa tetesi hizo.

Afisa habari wa Timu hiyo ya Mbeya City Ndugu Frady Jackson  amedai kuwa taarifa zinazozungumzwa juu ya kuuzwa kwa wachezaji hao si zakweli kwani wao badao wanatambua kuwa wachezaji hao ni mali yao hasa kutokana na mikataba yao ambayo imeweka wazi juu muda gani mchezaji huyo ataichezea timu hiyo.

Amesema yeye  kwa upande wake kama msemaji wa Timu hiyo bado haja pata taaifa zozote juu ya  kuuzwa kwa wachezaji hao licha ya kuendelea kuzisikia  kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa.

Amesema klabu hiyo haijakataza kwa mchezaji yoyote kusajiliwa na Timu nyingine inayoshiriki Ligi kuu lakini zipo taratibu za kufuatwa ili mchezaji awe huru kuchezea timu niyingine au kusajiliwa kabisa nasi vinginevyo kama inavyo dhaniwa nna baadhi ya wadau.

Amesema hata kama mchezaji atasaini mkataba na club hiyo ya Simba na nyinginezo  lakini bado wao kama viongozi hawalitambui hilo kwani bado hakujafanyika mazungumzo yoyote kati ya Uongozi wa Simba na Mbeya City.
“Nikweli Ndugu Mwanadishi hatukatai  kwa mchezaji yoyote kusajiliwa na Timu nyinmgine lakini sikuna taratibu zake za usajili mchezaji hawezi tu akaingia makubaliano anTimu nyingine pasipo uongozi wa wetu kufahamu,”Alisema hafisa Habari huyo.

Club hiyo ya Mbeya kwa mara ya kwanza imeshiriki Ligi kuu Tanzania Bara 2013/14  na kuleta upinzani mkubwa katika ligi hiyo ambapo mpaka ligi inakwisha Club hiyo ilishika nafasi ya Tatu tofautinna Simba ambayo ilishika nafasi ya Nne.

Deus KasekeAlizaliwa Nzovwe jijini Mbeya na kuanza kucheza soka toka akiwa shuleni, na hata alipofika sekondari katika shule ya Kalobe alikua ni mchezaji wa kutumainiwa wa timu ya shule.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top