Uteketezaji wa aina yake |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) kitengo cha ushuru wa bidhaa na forodha Mkoa wa Mbeya kimeteketeza kwa kuzifinyanga na kisha kuloweka kwenye maji shehena ya Sigara aina ya SM mali ya Kmpuni ya TCC zenye dhamani ya zaidi ya sh mil 30 zilikuwa zinasafirishwa kwenda Zambia lakini zimerejeshwa nchini kwa njia ya magendo.
Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi Joseph Ruge ambaye ni meneja wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya amesema ukamataji wa biadhaa hizo ulifanyika January23 Mwaka huu kwa kulihusisha gari namba T 980 CBW huku tera lake likiwa na namba T445 BHF ambalo ni mali ya kampuni ya NAM Enteprises ya jiji Dar-es-salaamu ambalo lilitokea nchini Zambia likielekea jiji Dar-es-salaam likendeshwa na Benfred Kingi.
Meneja huyo amesema kuwa gari hilo lilikamatwa katika eneo la Iwambi jiji Mbeya likiwa na box 60 za sigara aina hiyo likiwa limetokea nchini Zambia ambapo inadaiwa kuwa gari hilo lilkuwa limapakia mizigo mingine vikiwemo vipodozi.
Aidha katika tukio la pili la linahusisha basi kampuni ya TSK lenye namba za usajili T779 CSN linalo fanya safari zake Tunduma kwenda jiji Dar-es-salaam lilikamatwa Machi 23 mwaka huu katika kijiji cha Igawa Wilayani Mbarali likiwa na limepakia box tatu za Sigara hizo likotokea Tunduma.
Ruge amesema kuwa kwwa muda mrefu Mkoa wa Mbeya umeku moja ya vichochoro vya kuingizia
bidhaa hizo hapa nchini kinyume cha taratibu na Mamlaka husika zimekuwa zikiendesha msako wa kuzikamata zikiwa tayari sokoni jamboambalo pengine ndilo lililo ishitua mamlaka hiyo iliyo amua kuzidhibiti kuanzia zinakoingilia.
Meneja huyo amesema kuwa mbali na dhamani hiyo ya Sigala lakini wameteketeza malia ambayo imezaliswa
nchini kwa lengo la kuuzwa nje ya nchi lakini zikarudishwa kimagendo kinyume cha sheria hali iliyo liingizia Taifa hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 33 fedha ambazo zingelipwa kama ushuru ambapo box 63 ndanbi kukiwa na katoni 25 kwa kila box moja.
Kwa upande wake Meneja Kampmini ya Sigara hapa nchini (TCC) Mkoani Mbeya Wiliam Wiliam ambaye ni masahuhuda wa zoezi hilo alisema kuwa sigara hizo ni harali kwa matumizi ya binadamu lakini ilitengenezwa kwa soko la nje hivyo kitendo cha cha kuzirejesha ndani ya nchini kutaka kuuza kwa faida kwa kubwa kwani zinapunguzo la kodi na kinyume cha sheria.
Akizungumzia uamuzu wa kuteketeteza shehana hiyo kwa kutumia njia ya kuvunja na kisha kuziloweka kwenya maji tofauti na utaratibu ambao umezoeleka ambao umekuwa ukitumiwa na kwenye mizigo ambapo TRA huchoma, Williamu alisema kwa mjibu wa sheria za mazingira za kimataifa hairusiwi kwani zingeweza kuadhiri afya wa watu hivyo njia ya kuzifinyanga,kisha kuziloweka na baadaye kuzifukia katika shimo la taka ndiyo sahaihi.
Mwisho.
Post a Comment