TANZIA!
Mwanamuziki Mkongwe nchini Tanzania, Muhidin Gurumo amefariki dunia leo hii
majira ya saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa
amelazwa kwa matibabu.
Kwa
muda mrefu Mzee Gurumo amekuwa akisumbuliwa na maradhi mpaka siku ya leo
alipotangulia mbele ya haki.
Hili
ni pengo kubwa katika muziki wa dansi nchini kwani kwa muda wote wa uhai
wake amekuwa akitoa mchango mkubwa katika kuuendeleza muziki huo.
Kifo
cha Gurumo kimewagusa wadau mbalimbali wanaopenda na wasiopenda muziki kutokana
na umaarufu wake mkubwa aliojingea kupitia kipaji chake kikubwa.
Mtandao
huu utaendelea kukupatia taarifa zaidi kadri muda unavyozidi kwenda.
Tafadhali
endelea kufuatilia kwasababu timu nzima ipo njiani kueleka nyumbani kwa
marehemu.
Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya Mzee Gurumo mahala pema peponi. Ameni.
Post a Comment