Jopo la Wataalamu toka Nssf Mbeya likiendelea na ujasili wa vikundi vya ujasilimali Kata ya Rujewa Wilayani Mbarali Mkoani humo. |
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ujasilimali cha Magea kilichopo Rujewa Mbarali Ndugu Bakheresa Mlaja akifafanua jambo juu ya wao kutambua fursa na kujiunga na Mfuko huo . |
Afisa Shughuli (Senior Oparations) toka Nssf Mbeya Ndugu Gerard Mkony akitoa maelekezo toka kwa mmoja wa wanakikundi ambao walifika kujiandikisha kwa lengo la kuwa wanachama wa mfuko huo. |
Na EmanuelMadafa,Mbarali
Jumla ya vikundi 41 vya Mbalimbali vya ujasilimali Katika
Mkoa wa Mbeya vimesajiliwa na kuingizwa uanachama na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii NSSF Mkoani Mbeya .
Akizungumza Wilayani Mbarali wakati wa usajili wa baadhi ya
Vikundi wilayani humo Afisa Shughuli Mwandamizi (Senior
Operations Officer)NSSF Mkoani Mbeya Ndugu Gerard Mkony amesema usajili wa vikundi hivyo ni moja ya
mikakati uliwekwa na Mfuko huo.
Amesema mpango huo unalenga kuzifikia sekta zisizo rasmi kwa
mkoa wa mbeya katika uchangiaji wa hiali
hasa kwa vikundi vya ujasilimali pamoja na wakulima walio katika vikundi.
Amesema mpango huo unatoa fursa kwa wanachama kuchangia na
kupata mafao mbalimbali kama matibabu pamoja kukopeshwa nyumba za bei
nafuu na fursa ya kupata mikopo yenye
riba nafuu .
Hata hivyo Afisa huyo amesema kuwa katika Kata ya Rujewa pekee
Wilayani Mbarali wameweza kusajili jumla ya wanachma 33 katika kikundi cha Magea chenye wanachama
55 ambao wanajihusisha na ujasilimali.
Hata hivyo amebain
isha kuwa mbali na mpango huo pia mfuko
huo umeweka Misingi mbalimbali ya
kuimarisha zaidi mpango wa maendeleo ambao utaraisisha shuguli mbalimbali za
kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na hali ya Umaskini nchini.
Mwisho.
Post a Comment