Na EmanuelMadafa,Mbeya
POLISI
Mkoani Mbeya inawashikiliwa raia 82 wa nchini Ehtiopia kwa kosa la
kuingia Tanzania bila ya kibali.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetoka juzi majira ya
saa mbili usiku katika Kijiji cha Busale Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.
Amesema,
uchunguzi wa awali umebaini kwamba raia hao wa kigeni waliingia nchini
wakitokea nchi ya Malawi baada ya serikali ya nchi hiyo kuwafukuza..
Amesema,
katika harakati za kukimbilia nchini Tanzania raia wema waliwaona na kutoa taarifa
kwa jeshi la polisi zilizofanikisha kuwatia nguvuni watu hao.
Amesema,
taratibu zinafanywa ili watuhumiwa kukabidhiwa kwenye idara ya Uhamiaji huku
akiwataka wageni wa kutoka nchi za nje kujenga tabia ya kufuata taratibu za
kisheria pindi wanapotaka kusafiri kwenda nchi nyingine.
Hata hivyo
Kamanda Msangi, ameendelea kuwaomba wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa
polisi mara wanawatilia watu mashaka dhidi ya vitendo vya uhalifu.
Mwisho
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Post a Comment