Lukas Mwampiki aliyekuwa katibu mwenezi Mbeya |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mbeya kimemvua nyadhifa zote
Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Mbeya mjini Lukas Mwampiki ambae ni Diwani wa Kata
ya Mwakibete.
Akizungumza
na Blog hii Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, John Mwambigija amesemakwamba
Mwampiki na mwenzie Jocob Kaluwa ambaye ni mjumbe wa kamati tendaji ya
Wilaya wamebainika kukihujumu chama kwa kuvujisha siri za chama nje.
Nyadhifa
alizovuliwa Diwani huyo ni Ukatibu Mwenezi wa Wilaya na nafasi ya
Uwenyekiti wa Ulinzi na Usalma Kanda za Nyanda za Juu Kusini huku Kaluwa
akiondolewa nafasi yake ya ujumbe wa kamati tendaji.
Mwampiki na
mwenzie licha ya kuvuliwa nyadhifa hizo pia wamesimamishwa kutoshughulika na
kazi za chama mpaka uchunguzi utakapokamilika na kwamba endapo watabainika
kuhusika na tuhuma hizo hatua za kinidhamu zitachukuliwa ikiwa na kuvuliwa
uanachama.
Mwambigija,
amesema Katibu Mwenezi huyo ametajwa kuhusika na usambazaji wa nyaraka za ofisi
nje kwa viongozi wa Kata kinyume cha utaratibu.
Amesema,
kitendo hicho ni utomvu wa nidhamu hivyo chama kimewavumilia lakini
kimefika mahala sasa ni vema kikawachukulia hatua za kinidhamu wahusika ikiwa
na kuvuliwa uanachama endapo tuhuma wanazokabiliwa nazo zitathibitika
kuwa ni za kweli.
Akizungumzia
sakata hilo la kuvuliwa uongozi Diwani Mwampiki, amesema kwa upande wake
hawezi kuzungumzia chochote kwani tayari yeye binafsi alishaandika barua ya
kujihudhuru kutokana na kuchoshwa na majungu na fitina zilizopondani ya chama
hicho.
Amesema,
katika barua hiyo alieleza jinsi alivyochoshwa na kukerwa na vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wenzake ambao wamekuwa wakiendekeza
majungu, fitina na chuki zisizokuwa na sababu yoyote ya msingi zaidi ni tamaa
na uchu wa madaraka.
Hata hivyo
akizungumzia sakata la kujiudhuru nafasi yake ya ujumbe wa
kamati tendaji ndani ya chama,Kaluwa amesema yeye ameamua
kujipunguzia madaraka aliyokuwa nao ndani a chama na kutoa nafasi kwa vijana
wengine kushika nafasi hizo.
Mwisho.
Post a Comment