MATUMAINI ya vijana dhidi ya chama
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Iringa mjini imeanza
kutoweka baada ya jana dereva boda boda zaidi ya 200
kuwazuia viongozi wa Chadema kupeperusha wala kufunika bendera za
chama hicho katika bajaji iliyobeba mwili wa dereva mwenzao Abisai Mdesa
.
Vuta nikuvute hiyo ilitokea majira ya saa 4Asubuhi
Mei 27 mwaka huu baada ya makada wa Chadema
kufika Chumba cha maiti katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Iringa wakiwa na bendera za Chadema kwa ajili ya kuwapa madereva
wa boda boda pamoja na kufunga katika bajaji iliyopaswa kubeba mwili
wa marehemu huyo bado bado msimamo wa boda bado ulionekana kupingana na
matakwa ya viongozi hao.
Vijana hao walionesha kupinga
msimamo wa makada hao wa Chadema kutoka kufunika bendera wa chama chao
katika jeneza la marehemu huyo wala kupeperusha bendera ya chama chao
katika msafara wa mazishi kwa madai kuwa chama hicho cha boda boda Iringa si
chama cha kisiasa na wala hakina ubia na Chadema .
Wakizungumza kwa jazba vijana hao
waendesha boda boda boda walisema kuwa wamesikitishwa
na kitendo cha Chadema kutaka kujipatia umaarufu kupitia mazishi ya dereva
mwenzao huyu hali wakitambua kuwa wao si sehemu ya
Chadema.
Walisema walikuwa tayari kuwashambulia kwa
kipigo makada hao wanne wa Chadema waliofika na bendera hizo
iwapo wangeshindwa kuwasikiliza na kuendelea na msimamo wao wa
kufunga bendera.
Mwenyekiti wa chama cha boda boda na
Bajaji mjini Iringa Joseph Mwambope aliwaeleza waandishi wa
habari kuwa hatua ya Chadema kutaka kujimilikisha msiba
huo ni kosa kubwa na kuwa wanachotambua kuwa marehemu hakuwa
kiongozi wa Chadema ila alikuwa ni mwanachama wa chama cha boda boda hivyo
mbali ya ndugu mwenye nafasi ya kuendesha mazishi hayo ni chama
cha boda boda na Bajaji pamoja na wasanii wenzake wa Mundu Sanaa Group na
sio chama chochote cha siasa.
"Tunaomba ieleweke kuwa chama cha boda
boda si chama cha kisiasa hivyo haturuhusu Chadema ama CCM
kuja na bendera za vyama vyao katika msiba huu japo
hatuwakatazi kuja na magari yao yakiwa na bendera za
vyama vyao ila sio kuleta bendera tufungi kwenye boda boda na
bajaji zetu "alisema Mwambope
Kuwa imekuwa ni kawaida ya Chadema na
vyama vingine kujipendekeza katika misiba ambayo wanahisi ina
waombolezaji wengi ili kutumia nafasi hiyo kujitangaza kisiasa ila
wakati wa kuuguza vyama hivyo huwa havitokei kuuguza.
"Huyu mwenzetu mbali ya kupata ajali ya
pikipiki kwa siku zaidi ya nne sasa alikuwa amelezwa
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na madereva tulianza kuchangishana
ili kumfanyia rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili .....sasa kama
Chadema ambao leo wanakuja na bendera wapo kwanini wasingetoa
usafiri wa kwenda Muhimbili kama si kutaka kuonekana sasa baada ya kifo"
Katika
hatua nyingine vijana hao wa boda boda walilazimika
kuzomea kada wa Chadema aliyepewa kuweka shada kaburini kutokana na
kushindwa kukabidhi ahadi yao ya mchango wa shilingi 25000 ambazo waliahidi
kwenye daftari la waombolezaji bila kutoa pesa hiyo .
Kijana
huyo enzi za uhai wake alikuwa ni mpenzi wa
Chadema ambae mara kadhaa alionekana kupanda juu ya miti mirefu na kufunga
bendera za Chadema .FRANCIS GODWINLOG
| Mmoja wa makada wa chama hicho amabye pekee ndiye alaiye ruhusiwa kuweka shada ambapo hata hivyo alijikuta katika wakati mgumu kutokana na zomea zomea ya vijana hao. |






Post a Comment