Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
TANZANIA, Taifa Stars imeshinda mechi ya pili mfululizo
nyumbani chini ya kocha mpya, Mholanzi Mart Nooij baada ya kuilaza 1-0 Malawi
katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Israel Nkongo
aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Jesse Erasmo wote wa Tanzania, Taifa Stars
ilikwenda mapumziko ikiwa tayari inaongoza kwa bao hilo.
Bao hilo lilifungwa na kiungo mkongwe, Amri Ramadhani
Kiemba wa Simba SC dakika ya 35 kwa shuti kali baada ya kupokea krosi pasi
nzuri ya mchezaji wa AS Cannes ya Ufaransa, Shomary Kapombe aliyekuwa anacheza kama kiungo wa
ulinzi katika mchezo huo.
Hata hivyo leo Kipa
Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC, alifanya kazi ya ziada dakika ya 86 baada ya
kupangua shuti kali la ndani ya boksi la Rodrick Gonani.
Mchezo huu ulikuwa maalum kwa kila timu kujiandaa na
mchezo wa marudiano wa hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye
makundi ya kugombea tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
Tanzania baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe na
Malawi ikitoka kuifunga 2-0 Chad, zote zitakuwa ugenini wikiendi hii kujaribu
kutafuta nafasi ya kusonga mbele.
Kikosi cha Tanzania leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Himid Mao, Edward Charles, Said Mourad, Joram Mgezeke/Kevin Yondan dk72, Shomary Kapombe, Simon Msuva/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk46, Erasto Nyoni/Frank Domayo dk76, Kevin Friday/Said Juma dk73, Amri Kiemba/Mwinyi Kazimoto dk73 na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Malawi; Richard Chipuwa, Moses Chabuvula/Francis Mulimbika dk79, Limbikani Mzava/Bashiri Maunde dk57, John Lanjesi, Foster Namwera, Philip Masiye, Young Chimodzi Jr.,Gabadinho Mhango, Chimango Kaira, Joseph Kamwendo/Frank Banda dk67, Atusaghe Nyondo/Robin Ngalande dk30.ombe kutoka wingi ya kulia.

Mwisho

Post a Comment