Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
Na EmanuelMadafa,Mbeya

Kutokana na Kushuka kwa bei ya zao la  kahawa katika soko la Dunia jumla ya Halmashauri Nne za Mkoa wa Mbeya zimetajwa kushuka kiuchumi katokana na kuibuka kwa hali hiyo.


Halmashauri zilizo athirika ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ,Halmashauri ya Mbeya ,Mbozi  na Rungwe ambazo kwa kiwango kikubwa zimekuwa zikitegemea zao hilo katika moja ya pato lake.


Katika Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ikielezea  mpango wa utekelezaji wa matokeo makubwa sasa BRN hususani katika sekta ya kilimo mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua ya kushuka kwa bei ya zao la kahawa katika soko la dunia kumeshusha kwa kiwango kikubwa makusanyo katika halmashauri hizo.


Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa bei ya kahawa katika soko la dunia ilishuka  kutoka shilingi  4,000 hadi 1000 kwa kilo hali ambayo iliwadhohofisha kwa kiwango kikubwa wakulima  wa zao hilo.

Amesema katika halmashauri ya Mbozi pekee imeathiriwa zaidi na hali hiyo  hasa kutokana kutegemea ushuru wa kahawa.


Amesema katika makusanyo ya sasa 2013/14 Halmashauri hiyo imekusanya Tsh,645,206,757.7 ambayo nisawa na asilimia 32 tu  ya lengo la kukusanya Tsh,2,000,000,000.00/  kwa mwaka.


Kufuatia hali hiyo  halmashauri hizo hususani Mbozi zimetakiwa  kuimarisha ukusanyaji kutoka vyanzo vingine  sanjali na kubuni vyanzo  vipya vya mapato. 
mwishoo.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top