![]() |
| Marehemu Mangwair Enzi za Uhai wake |
Na
Andrew Chale full Shangwe blog
MASTAA
mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio
maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ ,
litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samaki samaki
Spot) , Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza
na mtando huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo, Kareeem Omary
‘KO’ alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila
mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert – Kumbukumbu ya kifo cha Albert
Mangwe’.
Kareem,
aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani
litakuwa la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi
hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia.
“Nawaomba
wadau kujitokeza kuonesha upendo wa pamoja. Kumbukumbu kwa
mpendwa wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na
kuongeza kuwa, siku hiyo Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa
pamoja na mama mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem
aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja na kutoka kwa kundi la
Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair, JSqueezer, P
Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja na
Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9, Samir, Zombie,
President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika
siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu, Kareem
alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili maalum
ikiwemo ya Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha,
Kareem alisema katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya
saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani ikiwemo ya
kuimba na nyinginezo na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo
wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’ alifariki
dunia akiwa nchini Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama
Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi alizowahi shirikishwa na wasanii
mbalimbali nchini wakiwemo Professa Jay, Nuru, TID, Chidi Benz na wengine
wengi.








Post a Comment