Kikundi cha vijana wakristo katika
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wameharibu msikiti na kuweka vizuizi barabarani kwa
kutumia magurudumu ya moto mjini Bangui.
Shambulizi hili limekuja siku moja
baada ya wapiganaji wa Seleka, kushambulia kanisa kwa kutumia maguruneti na
risasi , huku watu kadhaa wakiuawa.
Waasi wa Seleka ambao ni waisilamu ,
wamekuwa wakipigana vikali na wapiganaji wakristo wanaojiita 'anti-balaka'
tangu mwezi Machi mwaka 2013.
Takriban robo ya watu wote nchini
CAR, wameachwa bila makao kutokana na vita.
Hapajakuwa na ripoti zozote kuhusu majeruhi
kufuatia mashambulizi dhidi ya msikiti katika mtaa wa Lakouanga mjini Bangui.
Taarifa kadhaa zilisema kuwa msikiti
huo ulikuwa bila watu wakati wa mashambulizi.
Msemaji wa jamii ya waisilamu wa
Bangui, Ousmane Abakar, aliambia shirika la habari la AP kwamba kwa miezi sita
iliyopita,waisilamu wamekuwa wakishambuliwa huku misikiti ikiharibiwa.
Shambulizi la Jumatano dhidi ya
kanisa lilisababisha vifo vya watu 15 na lilijiri baada ya mapigano katika eneo
la PK5 mjini Bangui.
Kasisi mmoja wa kanisa hilo, Jonas
Bekas, alifahamisha BBC kuwa wanajeshi wa kulinda amani waliwasili kuchelewa na
kukosa kuzuia mauaji.BBC SWAHILI











Post a Comment