| Wananchi wakiwa barabarani huku wakiwa wamepanga magogo kushinikiza kuonana na mkuu wa mkoa wa mbeya mara baada ya mwananchi mwenzao kugongwa na kufa papo hapo. |
| Wafiwa wakiwa wameweka kambi pembezoni mwa barabara kumsubiri mkuu wa mkoa wa mbeya |
| Mwili wa Marehemu ukiwa chini pembezo mwa barabara |
| Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza kwa msisitizo na wananchi hao. |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza kwa kuwasihi wananchi hao kutotumia sheria mkononi. |
| Shughuli za kutoa vizuwizi zikiendelea mara baada ya mkuu wa mkoa kumaliza kuzungumza nao |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WANANCHI wa kijiji cha Nanyala Wilayani Mbozi, leo wamefunga
barabara kuu ya Tanzania- Zambia zaidi ya masaa matano na
kusababisha kukwama kwa wasafiri waendeo nchi za kusini mwa Afrika na jijini
Dar es Salaam.
Wananchi hao ambao waliamua kutumia
maiti ya mtoto wa miaka mitano Alfani Dumu ambaye aligongwa na gari ndogo ya
abiria (HICE) kwa kuilaza barabarani hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa
watumiaji wa njia hiyo.
Wakizungumza kwenye eneo la tukio, walisema tukio hilo
limetokea majira ya saa tatu za asubuhi mara baada ya marehemu mtoto huyo akiwa
anavuka barabara akitokea shuleni kugongwa na gari hilo.
Akielezea sababu ya wao kufunga
barabara hiyo, Mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema wamechoshwa na ahadi hewa za serikali
kwa kushindwa kuwatekelezea ombi lao la kuiweka barabara hiyo matuta,
alama za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani ambaye atakuwa
na tochi.
Amesema Zaidi ya miaka mitatu wamekuwa
wakipigia kelele suala hilo lakini hakuna utekelezaji wa aina yoyote
uliofanyika .
tumeiomba serikali kuangalia
uwezekano wa eneo hili la barabara
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, amewataka wakazi hao kuondoa maiti hiyo kisha
kufungua njia ili watumiaji waweze kuitumia kwani suala lao amelipokea na
kwamba atalifanyia kazi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo kuhakikisha linaweka askari wa usalama barabara kwa muda wote katika eneo hilo pamoja na kuhakikisha kuwa askari hao wanakuwa na vifaa vya kupimia mwendo kasi.
Amesema kwa dereva yoyote atakaye kwenda kinyume na taratibu ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo.
Aidha, Kandoro amemuagiza Wakala wa
barabara nchini(TANROAD) Mkoa wa Mbeya, kulifanyia matengenezo eneo hilo
kwa kuweka matuta pamoja na alama za barabarani mapema kesho badala ya kuchukua muda mrefu.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi, aliwahakikishia usalama wakazi hao na kwamba askari wa
tochi watakuwa kwenye eneo hilo huku akiwasisistiza kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi mara vitendo vya uhalifu vinapotokea.
Hata hivyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzungumza na wananchi haio na kuwasihi kufungua barabara hiyo mara moja wananchi hao walitii agizo hilo na usafiri kuendelea kama kawaida majira ya saa3 jioni.
mwisho







Post a Comment