Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
KIINGILIO cha chini cha mechi ya kirafiki kati ya
Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames) itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale
watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP
B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni ili kutoa fursa
kwa washabiki wengi zaidi kwa vile
itakuwa siku ya kazi.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo ya mechi kutoka Tukuyu mkoani Mbeya ambapo
imepiga kambi yake chini ya Kocha Mholanzi Mart Nooij.
Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani
Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotumiwa na timu
zote kama maandalizi ya mwisho kwa ajili mechi za mchujo za Kombe la Afrika
(AFCON).
Wakati Stars kwenye mechi za AFCON itarudiana na Zimbabwe
jijini Harare, Flames nayo itakuwa ugenini N’djamena kukabili Chad.
MWISHO.







Post a Comment