Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mmoja wa wadau wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphans Center kilichopo Uyole jijini Mbeya  akikabidhiwa cheti kama sehemu ya  shukrani kwa kuonyesha ushikirikiano kwa kituo hicho.








Na EmanuelMadafa,Mbeya

Licha ya Asasi kuweka nguvu katika kusaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo hususani jukumu la kulea watoto yatima  Mkoani Mbeya bado serikali imetajwa kuwa nyuma katika kuzisaidia asasi hizo.


Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Mkurugenzi wa wa Asasi ya kiraia ya Nuru Orphans Center Ndugu Jasson Mark wakati sherehe za kukabidhi vyeti na vitendea kazi kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wamehitimu katika chuo cha Ufundi  Veta jijini Mbeya kwa kufadhiliwa na kituo hicho.


Akizungumza amesema kwa asilimia kubwa ya watoto  wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Nuru Orphans Center  wengi wao hulepelekwa na serikali kupitia Idara ya Polisi  na Ustawi wa jamii.


Amesema pamoja na watoto na kituo hicho kuwapokea watoto hao  lakini bado serikali imekuwa ikishindwa kutoa mchango wake kwa uongozi wa kituo hicho ili kusadia malezi likiwemo suala la maradhi.


Amesema jukumu kubwa la kuwalea watoto hao limeachiwa kwa viongozi na wanachama na baadhi ya wasamalia wema ambao wamekuwa wakijitoa katika kutoa chakula na baadhi ya mahitaji mengine.



Hata hivyo amesema  ubalozi wa Japani Nchini ulitoa msaada kwa kituo hicho katika eneo la ujenzi wa Mabweni zaidi ya shilingi mil13  lakini bado halmashauri ya jiji la Mbeya  imeshindwa kuwasilisha  mchango huo.


 Kufuatia hali hiyo Uongozi wa kituo hicho  umetoa wito kwa serikali kuhakikisha inatoa ushawishi kwa Halmashauri  za mkoa huo kuhakikisha zinaajiri watumishi watakao kuwa na jukumu la kulea watoto yatima ili kupunga mzigo kwa vituo hivyo. 

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top