Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mabingwa wa U miseta kwa upande wa Mpira wa Miguu Halmashauri ya Kyela wakishangilia mara baada ya kuichabanga Halmashauri ya Mbeya 3.0  katika viwanja vya shule ya ufundi ya Iyunga. 





Wachezaji toka Halmashauri ya jiji la Mbeya wakishangilia kwa staili ya kaka zao Mbeya City Fc mara baada ya kuiadhibu Rungwe kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1 katika mashindano ya Umiseta ngazi ya Mkoa wa na kuwafanya kushika nafasi ya Tatu kwa mchezo wa mpira katika mashindano hayo

Kaimu Aisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu Jumma Mwaigombe 

Na EmanuelMadafa,Mbeya

Wito umetolewa kwa wakurugenzi  Halmashauri za Mkoani Mbeya kuhakikisha wanaendelea kulinda maeneo maalumu yalitengwa kwa ajili ya matumizi ya michezo.


Aidha sanjali na kulinda maeno hayo pia wakurugenzi hao wametakiwa kuacha tabia ya kutoa maeneo hayo kwa ajili ya wawekezaji .


Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu Jumma Mwaigambe wakati akifunga rasmi Mashindao ya Umiseta ngazi ya Mkoa katika viwanja vya Shule ya Ufundi ya Iyunga.


Afisa Elimu huyo amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi katika halmashauri hizo ambao wamekuwa wakijiuhusisha na uzaji wa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya matumizi ya michezo.


Amesema maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya michezo yamepokonywa na watu wanaodai kuwa ni wawekezaji huku viongozi wa Halmashauri hizo wakiwa kimya bila kutoa kalipio u zuio hasa kwa kutokana na kujali maslahi binafsi.

Aidha amedai kuwa zipo Halmasahuri ambazo zimeanzisha miradi ya maendeleo katika viwanja vya michezo hali ambayo imekuwa ikiwanyima fursa vijana kupata maeneo kwa ajili ya kuchezea mpira na michezo mingine.


Kufuatia hali hiyo Kaimu Afisa Elimu huyo amewataka wakurugenzi hao kuhakikisha maeneo yote yalovamiwa na watu yanalejeshwa pamoja na kuyaendeleza kwa ajili ya shughuli za michezo.


Katika Mashindano hayo teyari Mkoa wa Mbeya umekwisha unda kikosi kitakacho shiriki katika mashindano ya Umiseta ngazi ya Kanda kwa kushirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi.


Hata hivyo bingwa wa jumla wa mashindano hayo kwa michezo ya jumla ni Mbeya jiji wakifuatiwa na Kyela katika mchezo wa Mpira wa miguu . .

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top