Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro


Na EmanuelMadafa,Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinasimamia vyema ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato  vya ndani kwa lengo la kupunguza utegemezi kwa serikali kuu.

Mbali na kuongeza kasi ya ukusanyaji huo pia zimetakiwa kuongeza mchango wake  katika miradi ya Maendeleo inayoibuliwa na Wananchi.
Akizungumza jijini Mbeya Mkuu huyo wa Mkoa wa mbeya amesema kuwa kwa mwaka 2013,14lengo ni kukusanya  jumla ya shilingi 28,117,063,902 kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Kandoro amesema Halmashauri za Chunya ,Busokelo,Kyela,Mbeya jiji ,Mbeya na Ileje  zimekusanya zaidi ya asilimia 50 hali ambayo inaridhisha tofauti na Momba na Mbozi Rungwe  ambazo zipo chini ya asilimia 50.

Kufuatia hali hiyo ,Mkuuu huyo wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia vyema jukumu hilo la ukusanyaji wa mapato sanjali na matumizi yake.

Amesema kuwa nivema pia viongozi hao wakazuia uwepo wa mianya ya  upotevu wa mapato kupitia mikataba ya mawakala ambao wamekuwa wakizilazimu Halmashauri kuvunja mikataba na kuanza upya kukusanya fedha kutoka katika vyanzo vyake hali ambayo imekuwa ikisababisha hasara kubwa kwa Halmashauri hizo.

Wakati huo huo Kandoro amewataka wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na wakuu wengine wa Idara mbalimbali kuhakikisha wanapunguza safari zisizokuwa na ulazima ambazo zimekuwa zikighalimu kiasi kukubwa cha fedha hasa kwa  mazingira ya kudai posho.

Amesema katika bajeti ya 2013 ,14 kamati za bunge zimeagiza kuwa asilimia 60 ya makusanyo ya ndani lazima zitumike katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo  ndani ya halmashauri hizo hivyo lazima viongozi hao wakawa makini katika mipango yao ya matumizi ya fedha hizo.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top