![]() |
| Mwamuzi wa Mshindano hayo Ndugu Oscar Firbet akiapa mbele ya mgeni rasmi |
![]() |
| Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya Ndugu Costantine Mushi Akizindua Mashindano kwa ishara ya kupiga langoni. |
Na EmanuelMadafa,mbeya
Serikali Mkoani Mbeya, imewataka waandaji wa mashindano ya Umiseta na Umitashumta kutumia utaratibu wa kikanda kwenye mashindano hayo ngazi ya kitaifa ifikapo mwaka 2015.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu Juma Mwaigambe,ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umiseta Ngazi ya Mkoa katika viwanja vya shule ya Ufundi Iyunga.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu Juma Mwaigambe,ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umiseta Ngazi ya Mkoa katika viwanja vya shule ya Ufundi Iyunga.
Amesema Mchakato uliopo kwa sasa
ni kuanda timu ya pamoja kwa kushirikisha Halimashauri 10 za mkoa ambazo
zitapambana na Mikoa ya Rukwa na Katavi na kupata kikosi ambacho kitashiriki
fainali hizo.
Amesema hatua hiyo
inainyima fursa Mkoa wa Mbeya kushiriki
michuano hiyo hasa kutokana na Mkoa huo kuwa na Halmashauri nyingi ambazo
zinashiriki michuano tofauti na Katavi na Rukwa zenye Halmashauri chache.
Amesema mkoa wa Mbeya
unahalmashauri 10 zinazoshiriki mashindano hayo tofauti na Mikoa ya Rukwa na
Katavi ambayo inahalmashauri Chache hivyo nivema waandaji wa mashindano hayo
ngazi ya Tifa wakaliona hilo.
Amesema Teyari Mkoa wa Ilala
,Temeke na Kinondoni zimepewa fursa hiyo ya kuwa kanda maalumu ya kimichezo
hivyo umefika wakati sasa na Mkoa wa Mbeya ukapewa heshima hiyo.
Wakati huo huo Kaimu Afisa Elimu
huyo amesema kuwa bado mashindano hayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto
kubwa ya uhaba wa fedha .
Amesema kwa kiwango kikubwa
mashindano hayo yamekuwa yakiendeshwa kwa kutegemea fedha za ada za wanafunzi
ambao hata hivyo upatikanaji wenye wa ada umekuwa wa kusuasua.
Aidha kwa upande wake Afisa
Utamaduni Mkoa wa Mbeya Ndugu Goerge Mbigima amesema muitiko wa mashindano
hayo kwa mwaka huu umekuwa mkubwa tofauti na mwaka jana.
Mashindano hayo ya Umiseta ngazi
ya Mkoa yanafanyika ngazi ya Mkoa ambapo Halmashauri 10 za Mkoa zimeweza
kushiriki Mashindano kwa lengo la kupata kikosi kitakacho shiriki Mashindano ya
Kanda ambapo michunao hiyo itafanyika Mkoani hapa.
Mwisho
![]() |
| Afisa Utamaduni Mkoa Mbeya George Mbigima |
![]() |
| Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu Jumma Mwaigambe |
Mwisho.

















Post a Comment