Mtumbwi uliotumiwa na wanafunzi hao . |
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Campus ya Mbeya Prof.Ernest Kihanga akitoa maelezo juu ya vifo vya wanafunzi hao. |
Waziri Mkuu wa Serikali ya chuo hicho Ndugu Walioba Marato |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WANAFUNZI
wawili wa Chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya, wamepoteza maisha baada ya kuzama
kwenye bwawa la maji la kunyweshea wanyama lililopo kwenye hifadhi ndogo ya
Bonde la Ifisi Wilayani Mbeya.
Bwawa hilo
linamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Uinjilist lililopo eneo la Mbalizi,
limetengenezwa kwa ajili ya matumizi maalum ya kuhifadhi maji ili kutumika
nyakati za kiangazi kwa ajili ya wanyama ambao wamehifadhiwa kwenye bonde hilo
kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiutalii.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkuu wa Chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya, Profesa Ernest Kihanga, amesema
uongozi ulipata taarifa majira ya saa kumi jioni ya kwamba wanafunzi wawili
ambao ni Maiko Tarime na Albart Shenkalwa wote wamezaliwa katika miaka ya
1991 na 1992.
Amesema,
Marehemu Maiko anaishi Mkoani Tabora huku marehemu Albart ni mkazi wa Tanga
ambao wote kwa pamoja wanatarajiwa kusafirishwa leo(jana) kuelekea nyumbani
kwao kwa ajili ya maziko.
Akielezea
tukio hilo, Kihanga amesema wanafunzi hao ambao inasemekana walikuwa 14 wanaume
kwa wanawake waliongozana kwa pamoja na kwenda kwenye hifadhi hiyo kwa ajili ya
kuangalia wanyama mara baada ya chuo hicho kufungwa kwa muda wa wiki moja.
Amesema,
imeelezwa kwamba baada ya wanafunzi hao kuingia kwenye bwawa hilo la maji
wakitumia Mitumbwi na Boti zilizokuwa pembeni ndipo boti ilipinduka na marehemu
Maiko kuanza kuzama.
Kwa upande
wake Waziri Mkuu serikali ya wanafunzi, Warioba Marato, alisema kuwa wanafunzi
wamepokea taarifa ya msiba kwa mshtuko na kwamba wameushukuru uongozi wa chuo
hicho kwa kutoa ushirikiano kuanzia tukio lilipotokea hadi hatua ya mwisho ya
kuhakikisha miili hiyo ikisafirishwa nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.
Naye
Katibu Mkuu wa kanisa la Uinjilist Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole,
alisema kuwa wanafunzi hao wakiwa na wenzao wakike wapatao 14 walifika
kwenye kituo hicho kwa ajili ya kutembelea wanyama mbalimbali ambao
wemehifadhiwa kwenye hifadhi hiyo.
Amesema,
wakati wanafunzi hao wakitembezwa na muhusika wa kituo walifika kwenye bwawa
hilo la maji na kutaka kuingia ndani ya maji kitendo ambacho kilizuiliwa na
mmoja wa watumishi kwenye hifadhi hiyo.
Amesema,
Kwa mujibu wa msimamaizi huyo wa kituoa, wanafunzi hao walikuwa ni wabishi
hivyo wanafunzi wawili waliingia ndani ya Boti huku wanafunzi zaidi ya nane
wakipanda mtumbwi ikiwa ni kinyume cha utaratibu huku wakicheza na kurusha maji
ovyo.
Amesema,
Boti hiyo ilipinduka ndipo marehemu Maiko alipozama na marehemu
Albart
alipomuona mwenzake anazama ndipo alipoingia ndani ya maji kwa ajili ya
kumuokoa ambapo jitihada hizo ziligonga mwamba na wote wawili wakijikuta
wakipoteza maisha.
Aidha,
uongozi wa Kanisa hilo umesikitishwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea
tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo ndogo na kwamba limetoa pole kwa ndugu na
jamaa waliondokewa na ndugu zao.
Hata
hivyo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msani alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa
uongozi wa Chuo kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Mwisho.
Post a Comment