![]() | |
| Mbunge jimbo la Mbarali CCM Mheshimiwa Dickson Kirufi mwenye suti nyeusi aliyesimama akiwa ndani ya kikao cha Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mbeya. |
![]() |
| Wananchi nao hawakuwa nyuma katika kikao hicho |
![]() |
| Mbunge Kirufi akizungumza katika kikao hicho. |
![]() |
| Mwananchi akiwa nje ya ukumbi kusubiri kusikiliza kikao. |
Na EmanuelMadafa,mbeya
Katika hali isiyokua ya kawaida
Baadhi ya Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wameingia
katika mgogoro na Mbunge wa Jimbo hilo Dickson Kirufi mbele ya Mkuu wa Wilaya, Gulamhussein
Kifu katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Mbunge
huyo kuhoji malipo ya fedha za mawakala wa ushuru kwenye halmashauri hiyo
wakati yeye ni mjumbe wa kamati ya fedha, mipango na uchumi ambayo ndiyo
iliyohusika na jukumu la kuwapitisha mawakala hao.
Kikao hicho ambacho kilikuwa
kikipitia , kujadili na kufafanua,ajenda moja ya suala la ushuru wa zao la
mpunga ambapo hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya mawakala
wa kukusanya ushuru wa mpunga na wakulima mashambani ambao wamekuwa wakigomea
utaratibu huo.
Hatua hiyo ya madiwani kumzomea
mbunge wao inadaiwa ni kitendo cha mbunge huyo kuhoji suala hilo,
wakati yeye ni mjumbe wa kamati ya fedha , mipango na uchumi ambapo
alipaswa kufanya hivyo katika vikao vya kamati na si kwenye baraza.
Baada ya mbunge huyo kupewa nafasi
ya kuchangia hoja katika ajenda hiyo ya ufafanuzi kuhusu ushuru ,
katika hali isiyotarajiwa alianza kuuliza kama mawakala waliopewa tenda hiyo ya
kukusanya ushuru wamelipa malipo ya awali kama sheria inavyoagiza.
Hali hiyo ilionekana kuwakera
madiwani hao ambao walianza kupaza sauti wakitaka Mwenyekiti wao kuwapa nafasi
ya kutoa taarifa, jambo ambalo lilipuuzwa na Mwenyekiti huyo na kusababisha
madiwani hao kuanza kuzomea.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Keneth Ndingo, alisimama na kuruhusu taarifa, ambapo diwani
wa kata ya Itamboleo, lwitiko Mwangosi (CCM), alihoji sababu za mbunge huyo
kuuliza swala hilo la malipo ya fedha za awali za mawakala wakati na yeye ni
mjumbe wa kamati ya fedha.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa
halmashauri alitumia kauli za busara kuwatuliza madiwani , huku akiendelea
kutoa nafasi kwa mbunge huyo kumalizia kuchangia katika ajenda.
Wakitoa maazimio yao katika
ajenda hiyo, madiwani hao kwa pamoja waliazimia kusitishwa mara moja zoezi la
ukusanyaji ushuru na kuweka utaratibu mpya wa namna ya kukusanya ushuru wa zao
hilo, ambapo sasa ushuru wake utatozwa kwenye mchele na si mpunga.
Zoezi hilo la ushuru lililokuwa
likitekelezwa na mawakala 10 , wanadaiwa kukiuka taratibu kwa kukusanya ushuru
hadi kwa wakulima ambao walikuwa wakisafirisha mazao yao kutoka shambani kwenda
kuhifadhi majumbani.
Walimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri hiyo kuitisha zabuni itakayowezesha kupatikana kwa mawakala wapya
wanne watakaoendelea na kazi ya kukusanya ushuru huo
Mwisho.

















Post a Comment