Na EmanuelMadafa,Mbeya
POLISI Mkoani Mbeya, inamshikilia mtanzania
mmoja Hamis Mwakalinga(29) mkazi wa eneo la Soweto Jijijini Mbeya, kwa tuhuma
za kuwapokea na kuwasafirisha wahamiaji haramu 17.
Akizungumza jijini Mbeya Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa
saba mchana eneo la Mwanjelwa stendi ya Tukuyu Kata ya Ruanda Jijini Mbeya.
Amesema, polisi walipata taarifa ya kwamba
mtanzania huyo yupo na wageni kutoka nje kwenye eneo hilo akihangaika
kuwasfirisha.
Amesema mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi
waliweka mitego na baadaye kumbaini mtuhumiwa huyo akiwa na wahamiaji haramu hao.
Kamanda Msangi, amemtaja mmoja wa raia hao kuwa ni Nyabeda Samsoni (32) ambaye
alikuwa na wenzake 16.
Aidha, amesema kuwa wahamiaji haramu hao
tayari wamekabidhiwa kwenye mamlaka husiaka ya uhamiaji.
Hata hivyo, Kamanda Msangi ameiomba jamii
kuondokana na tamaa zisizokuwa na ulazima kwani kitendo cha kuwapokea raia
wakigeni kwa kificho kinaweza kikaligharimu Taifa.
Mwisho
| Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |






Post a Comment