Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Usalama Tanesco Mbeya Ndugu Cyprian Lugazira akionyesha Mita ya umeme ambayo imechakachuliwa na Kishoka huyo kwa ajili ya kuingiza umeme kwa njia ya wizi Ndani ya Nyumba yake na kuusambaza kwa majirani zake na kuwatoza fedha.


Afisa  wa Tanesco akionyesha moja ya eneo lilitumika kusamabazia umeme kwa majirani kwa njai ya udanganyifu ambayo imekuwa ikifanywa na Mthumiwa huyo Ndugu Daud Mwantika ambaye kwa sasa amekamatwa na kufikishwa katika kituo cha kati ya Polisi jijini Mbeya kwa mahojiano.

Mkuu wa kitengo cha Oparesheni Tanesco Mbeya Daud Mkotya


Gari lilotumiwa na Mtuhumiwa huyo katika harakati zake


Mafundi Tanesco wakikata umeme ulioibiwa na mtu huyo

Meneja Tanesco Mkoa wa Mbeya Enginia Amos Maganga



Na EmanuelMadafa,Mbeya

Hatimaye Shirika la Ugavi wa Umeme Tanesco Mkoa wa Mbeya, limefanikiwa kumkamata mtu mmoja   ambaye inadaiwa kuwa ni Mwizi wa mafuta ya Transifoma kwa kipindi kirefu sasa.


Mbali na kuhusika na wizi huo, pia mtu huyo ambaye maharufu kwa jina la kishoka, inasemekana amekuwa akijitambulisha kuwa yeye ni injinia kutoka kwenye shirika hilo hivyo, amekuwa akiwaunganishia watu umeme na kuwatoza kiasi cha fedha.


Tukio hilo limetokea jijini Mbeya Mei 20 mwaka huu  majira ya saa10:30 za jioni katika eneo la Ituha Sae lililopo Jijini Mbeya, ambapo watumishi wa shirika hilo wakishirikiana na askari polisi walifanikiwa kumbaini  mtu huyo  na kumtia nguvuni.


 Mkuu wa usalama wa Mkoa Tanesco, Cyprian Lugazia, amemtaja mtu huyo kuwa ni Daniel Mwantika ambaye amekuwa akilisumbua shirika hilo kwa muda mrefu sasa.


Amesema, mbali na hilo kishoka huyo amekuwa akijitambulisha kuwa yeye ni injinia wa umeme kutoka shirika hilo hivyo huwachukua  vijana na kufungua transfoma na kuiba mafuta hali ambayo imekuwa ikilighalimu shirika ikiwa na jamii kukosa umeme kutokana na kuungua hovyo kwa transfoma hizo.


Amesema shirika hilo lipo kwenye oparesheni ya kuwabaini wahujumu wa nishati ya umeme na mafuta ya transfoma baada ya kushamiri kwa vitendo hivyo na kulitia hasara ya mabilions ya fedha shirika.


Amesema wakati wapo katika masako huo walifanikiwa kupata taarifa ya mtu huyo amekuwa akilihujumu shirika kwa kuiba umeme nyumbani kwake na pia amekuwa akiwasambazia majirani wa eneo hilo na kuwatoza fedha pamoja na kuchukua malipo ya ankra.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Tonya Ituha Kata ya Ilomba Ndugu Jackson Mdemwa amesema tukio hilo la kukamatwa kwa mhalifu huyo nik tukio la kwanza kutokea katika eneo hilo.


Kufuatia wizi huo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya Enginia Amos Maganga Amesema  Katika kipindi cha mwaka mmoja shirika hilo  limepata hasara ya shilingi milioni 600 kutokana na kuungua kwa transfoma 12 huku wizi wa umeme ukigharimu kama milioni 400.


Amesema, uharibifu wa miundombinu wa shirika la umeme umeendelea kukua kwa kasi kubwa hivyo ameiomba jamii kutoa ushirikiano na kwamba kutokana na tukio hilo shirika limemsimamisha kazi kibarua ambaye alikuwa na jukumu la kusoma mita katika eneo hilo.

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top