![]() |
| Afisa Mahusiano Mamlka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA) |
Na Ukurasa
wa Mtukio
MAMLAKA ya
Maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya(mbeya uwsa) imebaini kuwa upotevu wa maji
uliokithiri ndani ya mamlaka hiyo unatokana na baadhi ya Wateja wao
kujiunganishia kinyume na taratibu.
Wateja hao
ambao Miongoni mwao ni pamoja na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ijulikanayo
kwa jina la Nyanga Bar and Guest House iliyopo Uyole jijini hapa wamebainika
kukutwa na kosa hilo katika oparesheni ya Nyumba kwa Nyumba ya kubaini wateja
wanaoiba maji inayoendelea.
Afisa Mahusiano Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira jijini mbeya (Uwsa) Ndugu Neema Stanton amesema hali imejitokeza mara baada ya kuanza kwa oparesheni maalumu kwa lengo la kubaini watu wanaolihujumu shirika hilo.

Kwa mujibu
wa afisa habari wa Mbeya UWUSA Neema Stanton wateja hao ambao majina yao
hayakutambulika mara moja kwakuwa hawakukutwa eneo la tukio jana wakati
oparesheni ikifanyika wamepewa agizo ya kujisalimisha katika ofisi hizo ifikapo
Mei 16 mwaka huu.
Stanton amesema wateja wengine saba nyumba zao ziko katika mtaa wa Mayombo uliopo katika eneo la Iwambi jijini Mbeya ambao makosa yao yalibainika wakati oparesheni ilipofanyika mtaani kwao.
Amesema mbali na mikakati ya oparesheni hiyo inayoendelea,taarifa za wasamaria wema zilizotokana na mamlaka kutoa ahadi ya kumzawadia shilingi 50,000 papo hapo mtu anayefanikisha kukamatwa kwa mhalifu yeyote wa hujuma dhidi ya mamlaka zimechangia kubainika kwa wateja hao.

Amesema kwa
mujibu wa sheria ya mamlaka mtu yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna yeyote
na wizi wa maji kwa kujiunganishia mtandao wa maji pasipo idhini ya mamlaka
adhabu yake ni ama kutozwa adahabu ya malipo ya shilingi milioni tano au
kifungo cha miaka mitatu jela na wakati mwingine adhabu zote mbili kwa pamoja.
Hata hivyo Afisa
Mahusiano huyo amesema oparesheni hiyo ni endelevu na itakuwa ikifanyika kwa
kushitukiza katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mbeya na kuwataka raia wema
kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa watu wanaokiuka
taratibu za mamlaka.
mwisho

Post a Comment