![]() |
| Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
MWANAFUNZI wa darasa la nne Dorris Yuko mwenye umri wa
miaka 12 amepoteza maisha baada ya kubakwa na kisha kunyongwa
shingo na binamu yake aitwaye Kenedy Elieza.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema tukio
hilo limetokea juzi majira ya nne usiku katika Kijiji cha Matwebe Kata ya Kikole
Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Msangi amesema, marehemu alikuwa
amelala ndani na wadogo zake wawili katika nyumba ya bibi yao ambaye kwa wakati
huo alikuwa amesafiri kuelekea Jijini Dar es Salaam.
Amesema, mtuhumiwa huyo ambaye ni binamu wa marehemu inasemekana
alipitia dirishani kisha kuingia ndani ya chumba walicholala watoto hao na
kufanya unyama huo.
Aidha, Kamanda Msangi amesema inasemekana mtuhumiwa
alifanikiwa kukimbia mara baada ya kufanya tukio hilo hivyo anatafutwa na
polisi.
Wakati huo huo, Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya
Sekondari Mpanda Panda Pilly Kasebele(18) mkazi wa kijiji cha Ilundo
Wilayani Rungwe, amepoteza maisha na kisha mwili wake kukutwa umetupwa kando
kando ya barabara.
Mwili wa marehemu mwanafunzi huyo ulikutwa kando kando ya barabara
hiyo mnamo tarehe 28/05/ 2014 majira ya tano za usiku katika Kijiji cha Kiwira
Wilayani Rungwe.
Kamanda Msangi amesema kuwa , uchunguzi wa polisi umebaini kuwa
marehemu huyo alikuwa akijaribu kutoa mimba.
Aidha, katika tukio hilo polisi linamshikilia Mwalimu wa shule
hiyo Tukundonda Kiluswa(27) baada ya kuhusishwa na mauaji hayo.
Hata hivyo Kamanda Msangi alisema, Mwili wa marehemu umefanyiwa
uchunguzi wa kitabibu na kutolewa kiumbe cha mtoto akiwa na umri wa miezi minne
jinsi ya kiume.
Mwisho.







Post a Comment