Mkuu wa Wilaya ya Kyela Esthar Malenga |
Na Mwandishi wetu ,Kyela
UTATA umegubika
mazingira ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu saba, raia wa Ethiopia waliokamatwa
Mei 14 mwaka huu katika kijiji cha Katumba Songwe, Wilayani Kyela.
Hatua hiyo inatokana na taarifa ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bugema ya pili katika kijiji hicho cha Katumba Songwe, Boniface Mwakilima, kudai kuwa wahamiaji hao haramu walikamatwa ndani ya nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji hicho.
Akizungumza na Blog hii kwa sharti la kutopigwa picha Mwenyekiti huyo wa kitongoji alisema kabla ya wahamiaji hao kukabidhiwa mikononi mwa polisi, walikamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika moja ya chumba katika nyumba ya Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Juma Mwabungulu.
Amesema wao kama
viongozi, walipokea taarifa za siri za kuhifadhiwa kwa wahamiaji hao haramu
nyumbani kwa Mwenyekiti wao Mei 13 Mwaka huu na kuanza uchunguzi wa kubaini
ukweli wake.
Ameongeza kuwa
baada ya kuona hali hiyo waliwasiliana na mtendaji wa kijiji hicho, Roya
Mwakilambo, ambaye aliita askari mgambo wa kijiji na kwenda kufanya ukaguzi.
Mwakilima ameongeza
kuwa,baada ya kufika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo walimtaarifu juu ya ukaguzi
huo, lakini katika hali isiyo ya kawaida aligomea moja ya chumba kwa madai
wasingeweza kukifungua kwa kuwa ni cha mwanae ambaye alikuwa amesafiri.
Ameongeza kuwa
hawakukubaliana na pingamizi hilo na walivunja mlango huo na kukuta wahamiaji
hao wakiwa wamefichwa, huku hali zao zikiwa dhaifu, hivyo waliwachukua hadi
ofisi za kata na kutoa taarifa polisi.
Hata hivyo, amesema tukio hilo ni la tatu kwa Mwenyekiti huyo, ambapo mwaka 2012 aliwahi kukutwa na wahamiaji haramu 80 na kesi yake ilifika mahakamani lakini akaachiwa huru .
Jeshi la polisi jana limetoa taarifa ya kumsaka mwananchi mmoja kwa tuhuma za kudaiwa kuwahifadhi wahamiaji haramu saba waliokamatwa katika kijiji cha katumba Songwe Wilayani Kyela.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga, alipoulizwa juu ya tukio hilo, alijibu kuwa kwa hasira kuwa yeye hafanyi kazi za serikali kwa simu.
Mwisho.
Post a Comment