Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariamu Mtunguja akitoa taarifa ya ugonjwa wa Dengue kwa waandishi wa habari |
Na EmanuelMadafa,Kyela
SERIKALI
Mkoani Mbeya, imewataka wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuondoa hofu juu ya ugonjwa
ulioibuka nchini wa Dengue
kwa kuwa mpaka sasa idara ya afya haijapokea kesi ya mtu aliyepatwa na
ugonjwa huo.
Akizungumzia
hilo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, alisema hadi sasa hakuna
mtu au mgonjwa aliyeripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Mtunguja,
alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuzagaa kwa uvumi kutoka kwa baadhi ya
wananchi ya kwamba ugonjwa huo tayari umebisha hodi Mbeya na tayari kunamgonjwa
amelazwa.
Amesema
taarifa zilizoenea mtaani zinajengwa na hofu tu na kwamba timu ya wataalamu wa
afya imeendelea kufanya kazi muda wote ili kuona kama kuna taarifa za kuwepo au
kutokea kwa mtu yeyote mwenye dalili au ugonjwa huo.
Amesema
tayari madaktari wa wilaya zote mkoani hapa wamepewa waraka unaotoa muongozo wa namna wa kushughulikia
kwa haraka taarifa zote zinazotolewa na wananchi juu ya mtu yeyote anayeonesha
dalili za kuwa na ugonjwa wa Dengue.
Mbali
na madaktari, lakini pia ofisi hiyo ya Mkuu wa mkoa imetoa agizo kwa wakurugenzi
wa halmashauri zote kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zote suala la usafi.
Kwa
upande wake, Mganga Mfawidhi kutoka hospitali ya mkoa wa Mbeya, Dk. Grolia
Mbwile, alisema licha Tanzania kukumbwa na ugonjwa huo ambao hata hivyo hauna
tiba wa kinga, lakini pia umewahi kuibuka katika nchi ya Misri barani Afrika ,
pamoja na nchi kadhaa katika bara la Asia.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na mtafiti wa tabia za mbu kutoka
Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), Dk . Nicholaus Govela alisema ugonjwa wa
Dengue unaambukizwa na mbu aitwae Aedes
Egypti.
Mwisho.
Mganga Mfawidhi Hospital ya Mkoa wa Mbeya Daktari Grolia Mbwile |
Post a Comment