Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Licha ya serikali kuendelea
kupambana na Vitendo vya uhamiaji haramu Nchini
mkakati huo unaonyesha kukwamishwa na baadhi ya watendaji wa serikali.
Hatua hiyo inakuja kufuatia
malalamiko toka kwa wananchi Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kuwa lalamikia baadhi
ya watendaji kuwa wamekuwa wakiwahifadhi wahamiaji haramu kinyume cha sheria.
Wakizungumza na Blog hii wakazi
wa wa Kata ya Katumba Wilayani Kyela,
wamesema kukithiri kwa vitendo vya wahamiaji haramu Mkoani Mbeya kumechangiwa
na baadhi ya watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakiwapokea na kuwahifadhi.
Wamesema, viongozi hao wamekuwa
wakiwasafirisha wahamiaji hao licha ya
serikali kutumia gharama kubwa ya kupambana na wimbi hilo la watu wanaoingia
nchini kinyume cha taratibu.
Wakizungumzia tukio la kukamatwa kwa raia saba kutoka nchini
Ethiopia lililotokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8:30 katika kijiji cha Katumba Songwe Wilayani Kyela ambalo
linadaiwa kuhusisha viongozi wa serikali.
Wamesema,wahamiaji hao waliingia
nchini kwa kupokelewa na kuhifadhiwa na kiongozi mmoja wa serikali Wilaya ya Kyela (jina
limehifadhiwa).
Habari za uhakika zinaeleza kuwa
kiongozi huyo amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo kwa muda mrefu hali
iliyoshindwa kuvumiliwa na wananchi na kuamua kumtaja hadharani.
Katika taarifa iliyotolewa jana
na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa jeshi hilo
linamtafuta mtu mmoja ambaye hata hivyo halikumtaja jina kwa tuhuma za kuwahifadhi wahamiaji haramu saba.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi, alisema raia hao saba kutoka nchini Ethiopia walikamatwa wakiwa
wamehifadhiwa na mtu huyo baada ya kupokea taarifa za raia wema.
Aliwataja raia hao haramu kuwa ni Michael Solomon (45) 2, Abebe Isako
(24), Adise Mashone (20) , Abraham Maniko (20) , Ocee Watino (26),Abraham Ganduu
(24) , Agram Gandule (26).
“Taratibu zinafanywa ili wakabidhiwe idara ya uhamiaji kwa
hatua zaidi, aidha jeshi la polisi linaendelea
kumtafuta mtu aliyewahifadhi wahamiaji hao ambae jina lake tunalihifadhi.” alisema.
Takribani miaka mitano sasa kumekuwa na wimbi kubwa la
wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia, Somalia, Burundi, Rwanda na Jamuhuri
ya kidemokrasia ya Kongo wamekuwa wakiitumia Tanzania kama mapito ya kuelekea
nchi za kusini mwa Afrika kusaka maisha bora.
Mwisho.
Moja wa Kundi la wahamiaji haramu wakiwa chini ya Ulinzi |
Post a Comment