Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariam Mtunguja akizungumza katika sherehe za siku ya wauguzi Duniani katika viwanja vya CCM Ilomba jijini Mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Serikali
Mkoani Mbeya imeonyesha kusikitishwa na
hatua ya baadhi ya watumishi wa idara ya afya Mkoa wa Mbeya kwa
kushindwa kulipwa posho za sare na masaa ya ziada kwa zaidi ya
miaka miwili.
Fedha hizo
hutengwa kwenye bajeti ya serikali kwa ajili ya malipo ya sare za
wauuguzi(Uniform allowance) ambapo kila mwaka muuguzi hulipwa shilingi 120,000
jambo ambalo katika halimashauri nyingine zimeshindwa kulitekeleza.
Malalamiko
hayo wameyatoa Mei 12 kwenye
risala yao iliyosomwa na Aqulina Mtweve, wakati wa maadhimisho ya siku ya
wauuguzi Duniani ambapo kwa Mkoa wa Mbeya yamefanyika katika viwanja vya Ruanda
Nzovwe Jijini Mbeya huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya,
Mariam Mtunguja.
Akionyesha
kustushwa na hali hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja
amesema serikali imekuwa ikiwasilisha fedha zote
kwenye mamlaka husika.
Amesema
suala la posho za sare na masaa ya
ziada limemchanganya kwani serikali imekuwa ikiwasilisha fedha zote na
wakati husika .
Aidha, amesema
kuwa fedha hizo zinapaswa kukabidhiwa kwa watumishi wenyewe si viongozi
kuchukua na kuwashonea wauguzi mavazi ambayo hawayapendi.
Awali
wakiwasilisha risala hiyo mbele ya mgeni rasmi Wamesema, fedha hizo hutolewa na
serikali kila mwaka lakini baadhi ya halmashauri ambazo walizitaja kwa
majina kuwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Halmashauri ya Chunya kuwa zimeshindwa
kuwalipa wauuguzi hao huku wakidai kuwa fedha hizo zikiingizwa kwenye matumizi
mengine.
Wamesema
hali hiyo inaonesha ni jinsi gani serikali ilivyowapuuza wauguzi kwa kushindwa
kutambua umuhimu wao kwa jamii.
Wakizungumzia
malipo ya posho ya masaa ya ziada(ETRADUTY), wauuguzi hao wamesema kuwa baadhi
ya halmashauri zimekuwa haziwalipi hali watumishi wengine
wanalipwa huku wakitolea mfano halmashauri ya Jiji la Mbeya na Chunya.
MWISHO.
Post a Comment