![]() |
| Wahitimu wakiserebuka kwa staili ya kwaito kufurahia sherehe hizo |
![]() |
| Wageni waalikwa katika sherehe hizo |
Na
EmanuelMadafa,mbeya
Serikali kupitia wizara ya Elimu na Mfunzo ya
Ufundi imetakiwa kubadilisha mfumo wa ufundishaji wa masomo ya Ukutubi ngazi ya
cheti ili kuweza kuendana na mabadiliko ya sasa ya kiteknolojia na utandawazi
uliopo sasa.
Kauli hiyo imetolewa na wahitimu katika chuo cha Ufundi cha Academy
Vocation Treaning Center kilichopo Kabwe jijini Mbeya wakati wakiti
wakikabidhiwa vyeti vya uhitimu katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa
Mkapa jijini humo.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa vyeti
hivyo baadhi ya wahitimu hao wamesema
kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa katika usomaji wa masomo ya fani hiyo hasa
kutokana na kusoma silabasi ambazo haziendani na wakati uliopo sasa.
Wamesema kuna baadhi ya masomo katika fani
hiyo hususani katika uchapaji wamekuwa wakitumia mashine za kizamani (typewriting
machine ambazo kama wataajiliwa au
kujiajili hawatoweza kuzitumia hasa kutokana na mfumo uliopo sasa wa Kidigiti
zaidi.
Mmoja wa wahitimu hao Ndugu Edithar Nziku
pamoja na Janeth Sanga wamesema shida kuwa ni pale mwafunzi anapo pata ajira na
kukutana mazingira ambayo yamekuwa yakiwapa shida hususani kwa kukutana na
vifaa vya kisasa vya ambavyo wao hawakupata fursa ya kuvisoma kipindi cha
masomo yao.
Pamoja na kuwepo kwa chnagmoto hizo pia
wanafunzi hao wamesema asilimia kubwa ya wanafunzi wanaomaliza katika chuo
hicho wamkeuwa na mafanikio makubwa mara wanapo pata fursa ya kuajiliwa na hata
kujiajili wenyewe hasa kutokana na kupewa mbinu mbalimbali za kiujasilimali na
walimu wao.
Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hich
Ndugu
Daines Mhoka amesema kuwa changamto kubwa wanayokutana nayo katika hatua ya
utoaji elimu kwa vijana hao ni uhaba wa baadhi masomo hususani somo la
Typewriting pamoja kutopatikana kwa mashine hizo .
Aidha amesema kuwa changamoto nyingine ni
uhaba wa maeneo kwa ajili ya kufundishia sanjali na ukosefu wa baadhi ya vifaa
vya ufundishaji wa masomo ya fani hiyo.
Jumla ya wahitimu 30 ngazi ya cheti
wamehitimu mafunzo katika chuo hicho na kupatiwa vyeti shughuli ambayo
iliendana na sherehe katika ukumbi wa mdogo wa mkapa jijini Mbeya.











Post a Comment