Na Mwandishi wetu,Dar es salaam
Hatimaye watanzania hii leo wameweza
kupata faraja mpya mara baada ya TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
kuifunga bao 1-0 Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa
kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2005
nchini Morocco, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na
refa
Joseph Odartei Lamptey aliyesaidiwa na Malid Alidu Salifu na David Laryea wote wa Ghana, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.
Joseph Odartei Lamptey aliyesaidiwa na Malid Alidu Salifu na David Laryea wote wa Ghana, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 13 akiunganisha kwa guu la kushoto krosi maridadi ya mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwwengu.
Kocha wa Tanzania, Mholanzi Mart
Nooij alisema baada ya mchezo huo kwamba vijana wake wamecheza vizuri, lakini
wangeweza kupata mabao zaidi kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza.
Kwa upande wake, kocha mzalendo wa Zimbabwe, Ian Gorowa
alisema vijana walicheza vizuri, lakini walikosa bahati ya kupata mabao licha
ya kutengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri,
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo/Amri Kiemba dk71, Mrisho Ngassa/Haroun Chanongo dk77, Mwinyi Kazimoto, John Bocco/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk85, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Zimbabwe;
George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen
Alimenda, Rendai Ndoro, Milton Ncube, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila,
Peter Moyo na Eric Chipeta.
Mechi
nyingine za zilizotarajiwa kuchezwa ni kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na
Guinea Bissau, Swaziland na Sierra Leone, Msumbiji na Sudan Kusini, Madagascar
na Uganda, Burundi na Botswana, Liberia na Lesotho, Kenya na Comoro na Libya vs
Rwanda.
Mechi
za marudiano zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Mei 30 na washindi
wataingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo ili kuwania kupangwa kwenye makundi
tayari kwa mbio rasmi za Morocco 2015.
mwisho.

Post a Comment