| Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gullam Husein Kifu mwenye shati la Drafti aliyesimama |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Wafanyabiashara wa zao la Mpunga Wilayani Mbarali Mkoani
Mbeya Wamegomea halimashauri hiyo kwa hatua yake ya kupitisha uamuzi wa kutoza
tozo mpya kwa zao hilo kutoka shilingi
1000 hadi 2000.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Halm ashauri hiyo kupitia baraza
lake la Madiwani kupitisha azimio la kuanza kutoza tozo mpya kwa wafanya
biashara wa zao hilo kutoka shilingi 1000 hadi shilingi 2000.
Pia mgomo huo wa Wafanyabiashara unatokana
na baadhi ya watendaji wa
Halmasahuri hiyo kuwatoza ushuru wafanyabiashara hao mara mbili kinyume
na taratibu.
Akizungumza wilayani Wilayani humo mkuu huyo wa wilaya ameonyesha kushangazwa
na hatua hiyo ya wafanyabiashara kugomea agizo hilo licha ya Halmashauri hiyo kupitia baraza lake madiwani kupitisha azimio hilo .
Amesema kumeibuka kwa kundi la baadhi ya watu ambao wamepanga
mkakati wa kutaka kukwamisha mpango huo kwa lengo la kuhakikisha halimasahuri
hiyo inasahindwa kujiendesha.
Amesema kwa asilimia kubwa halimasahuri hiyo inategema pato
lake kutoka kwenye kilimo hususani
kilimo cha mpunga hivyo kukwama kwa zaoezi hilo kutachangia kwa sailimia kubwa
Halmashauri hiyo kushindwa kijiendesha.
Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka
wafanyabiashara hao kuketi pamoja na kulijadili suala hilo badala ya kuendelea
kuleta msuguano usio na tija kwa
msakabari wa Halmashauri hiyo.
Hata hivyo Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji
Mdogo wa Rujewa Ndugu Festo Mkemwa amesema kuwa hatua ya wafanyabiashara hao
kugoma kulipa tozo hiyo mpya ya shilingi 2000 ni kukiuka sheria.
Pia amesema mgomo unaibuka wakati teyari mamlaka hiyo kupitia baraza lake la madiwani limekwisha
tunga sheria ndogo toka mwaka jana ikiambatana na utolewaji wa elimu kwa wafanyabiashara hao pamoja na
wananchi kwa ujumla.
Mwisho.






Post a Comment