Mganga Mkuu jiji la Mbeya Daktari Samuel Lazaro |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Licha ya serikali Mkoani Mbeya kutoa
tahadhari kwa wananchi wake juu hatarini
kukumbwa na ugonjwa wa Dengue bado idadi kubwa ya wakazi wa jiji la
mbeya wameonyesha kutotilia maanani suala hilo.
Utafiti uliyofanywa na blog hii umebaini kuwa asilimia kubwa ya wageni ambao
hutumia nyumba za kulala, hawatumii vyandarua wakati wa kulala hata wakati wa
kujipumzisha mchana kwa madai ya kwamba Mbeya kuna baridi hivyo ni vigumu kwa
mbu huyo kuishi kwenye eneo hilo.
Pia, bado wamiliki wa nyumba hizo
wameshindwa kuzidhibiti kwa kufukia maeneo mbalimbali ambayo yanaweza
kuwa ni mazalia ya mbu wa aina yoyote ile akiwemo Aedes ambaye ametajwa
kuuma mchana na ndiye anayeeneza homa ya ugonjwa huo.
Akizungumzia zaidi hali hiyo Mganga wa Mkuu wa halmashauri ya Jiji la
Mbeya, Dkt. Samweli Razalo, amesema changamoto kubwa wanayoipata ni jamii
kushindwa kutambua hatari ya ugonjwa huo kwani baadhi ya watu wamekuwa
wakipuuza vitu vidogo vidogo bila kufahamu ya kwamba vitu hivyo ndio
vyenye madhara.
Aidha, Razalo amesema, jamii ya majumbani
imekuwa na uelewa mdogo wa kujikinga na mbu huyo kwani licha ya kujidhibiti kwa
kuvaa nguo ndefu pamoja na kudhibiti mazalia ya mbu lakini bado wameshindwa
kutumia vyandarua mara wanapojipumzisha mchana.
Pia, ameongeza kuwa bado
kunachangamoto kubwa kwa wanafunzi wa kike waliopo kwenye vyuo vikuu
kwani kwa asilimia kubwa wameendelea kuvaa mavazi mafupi bila ya kutambua ya
kuwa wapo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na homo hiyo.
Amesema, ni kweli mpaka sasa Mkoa wa
Mbeya hauna taarifa yeyote iliyoripotiwa kuwepo kwa mgonjwa wala mtu aliyelazwa
kwa homa hiyo lakini ni vema jamii ikatambua madhara yake hivyo kuchukua
tahadhari .
Amesema tayari madaktari wa
wilaya zote mkoani hapa wamepewa waraka unaotoa muongozo wa namna wa
kushughulikia kwa haraka taarifa zote zinazotolewa na wananchi juu ya mtu
yeyote anayeonesha dalili za kuwa na ugonjwa wa Dengue.
Mbali na madaktari, lakini pia ofisi
hiyo ya Mkuu wa mkoa imetoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo
kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zote suala la usafi.
Hata hivyo,Kwa upande wake, Mganga
Mfawidhi kutoka hospitali ya mkoa wa Mbeya, Dk. Grolia Mbwile, alisema licha
Tanzania kukumbwa na ugonjwa huo ambao hata hivyo hauna tiba wa kinga, lakini
pia umewahi kuibuka katika nchi ya Misri barani Afrika , pamoja na nchi kadhaa
katika bara la Asia.
Mwisho.
Post a Comment