Nasikitika kwamba
katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za
majitaka.
Kampuni ya
LekaDutigite inamilikiwa na wasanii. Gombe Advisors ni kampuni isiyofanya faida
(Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara.
Wasanii wa Kigoma
wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo.(Martha
Magessa)
Leo mpigie simu
mfanyakazi yeyote wa NSSF utasikia kazi ya wasanii hao. Kwa namna yeyote ile
hii ni ishara ya kukosa ubinaadam maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote
ya kifedha Leo wala kesho kwa LekaDutigite na Gombe Advisors.
Kipindi ambacho
mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama chao, pole
ninayopewa ndio hiyo.
Hakuna namna ya
kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.
Zitto Zuberi
Kabwe: Hata hivyo, ni vema CAG afanye ukaguzi haraka sana na Mimi binafsi
nitawajibika iwapo itaonekana kwa namna yeyote ile nina maslahi ya kifedha
katika LekaDutigite na gombe advisors.
CHANZO:FRANCI
GODWIN







Post a Comment