| Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Na EmanuelMadafa,mbeya
Mkazi wa kijiji cha Mantengu Wilayani mbozi Mkoani
Mbeya Ndugu Wlliam Kabinji (38) amekutwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye
ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga sehemu za usoni na juu ya
jicho la kushoto kisha kunyongwa shingo na kutundikwa juu ya mti akiwa amefungwa shingoni kwa kutumia kitenge.
Tukio hilo limetokea June 08.06.2014 majira ya saa
12:00 mchana katika kijiji cha ilembo, kata ya vwawa, tarafa ya vwawa,
wilaya ya mbozi, mkoa wa mbeya.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed
Msangi amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuchoma moto nyumba tatu za jirani
zake na kuiteketeza kabisa nyumba ya elias mwamlima (32) mkazi wa kijiji cha
mantengu [a] tarehe 04.06.2014 majira ya saa 21:30 usiku na kutoroka.
Jitihada za kuwasaka na kuwakamata watu waliohusika na
tukio hili ambao ni majirani wanaofahamika zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi
mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi
anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni
kinyume cha sheria na badala yake wajenge tabia ya kuwafikisha watuhumiwa
wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za
kisheria.
Mwisho






Post a Comment