Shirika moja la misaada limeitaka
Facebook kurudisha fedha ilizopata kwa kufanya matangazo ya kampeni yake rais
Bashar al-Assad wa Syria.
Matangazo hayo- ambayo sasa
yametolewa na Facebook- yalianzishwa mwezi Mei , na yamehusishwa na ukurasa
unaoitwa Sawa al-Assad. Sawa ina maana ya “pamoja”, neno ambalo alitumia rais
huyo kama kauli mbiu wakati wa kampeni.
Utata umetokana na matangazo mengi
yanayoendelea kuukuza katika mtandao wa Facebook. Kwa kuwa matangazo haya
yalikuwa yamelipiwa, kampuni hiyo basi ilipokea fedha kwa matangazo hayo
yaliyoimarisha kampeni ya siasa zake Assad- jambo ambalo limelikera shirika la
kutoa msaada liitwalo ‘the Syria Compaign’.
Shirika hilo limetengeneza wavuti
unaoitwa 'AdsForDictators.org unaokejeli Facebook' na unatoa malalamishi kwenye
mtandao.
“Wanafanya pesa mbovu kuwa nzuri,”
John Jackson ambaye ni mkurugenzi wa shirika hilo aliiambia BBC. “Wanapaswa
kutoa pesa hizo kwa shirika la misaada lenye sifa ambalo linawashughulikia
wakimbizi wa Syria.”
Haijulikani ni pesa ngapi, ingawa
katika muda mfupi ambao tangazo hilo lilifanywa, kuna uwezekano kuwa ni kiwango
kikubwa cha pesa.
Facebook bado haijasema chochote
kuhusiana na jambo hilo, ila tu kusema kwamba tangazo hilo halikufanywa kutoka
Syria- jambo ambalo litavunja masharti yaliyowekewa taifa hilo- na kwamba “kama
kawaida sisi huondoa matangazo yasiyofuata kanuni zetu.”
Hata hivyo, haijulikani hasa ni
kanuni zipi walizokiuka. Hakuna kabila lililotumiwa ambalo lina uchochezi, na
pia matangazo ya kisiasa katika mtandao wa Facebook hukubaliwa.
Itakumbukwa kuwa kampuni hiyo
ilikuwa imeorodhesha mbinu za kuwasaidia waliokuwa wakigombea nyadhifa
mbalimbali mwaka wa 2012 nchini Marekani kupitia kwenye Facebook.CHANZO BBC SWAHILI







Post a Comment