Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Afisa wa Tanesco akionyesha lisiti ya malipo pamoja na Mita ambavyo vimekuwa vikitumika kimakosa na mmoja wa wateja wao ambaye inadaiwa ameunganishiwa umeme na Kishoka kaatika eneo la Kagera Ilomba jijini Mbeya.

Afisa  Usalama  Tanesco Mkoa wa Mbeya Ciprian Lugazia akitoa ufafanuzi juu ya kuwepo kwa wateja waliounganishiwa umeme na Kishoka .
Nguzo ya shirika la Mawasiliano TTCL ikiwa imetumika kama sehemu ya nguzo ya umeme kusambazia wateja feki.
 Picha na jamiimojablog


Na EmanuelMadafa.Mbeya
WATU wanne wanashikiliwa na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Mbeya,kwa tuhuma za kulihujumu shirika kwa kujiunganishia kinyume cha utaratibu.

Hatua hiyo imekuja zikiwa zimepita wiki mbili tangu shirika hilo kumkamata mkazi wa Ituha, Jijini hapa, Daniel Mwantika kwa tuhuma za kuliibia umeme shirika hilo na kuusamba kwa majirani zake huku akijitambulisha kuwa ni injinia wa shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha usalama Mkoani Mbeya, Cyprian Lugazia, alisema watu hao wanne walikamatwa katika maeneo tofauti Jijini hapa ambayo ni  Songwe, Ilomba, Kagera na Ituha.

Lugazia, ingawa hakuwa tayari kuwataja majina watu hao kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea , alisema zoezi hilo lilifanikiwa kutokana na taarifa za wasamalia wema.



Meneja wa Tanesco mkoa wa Mbeya, Injinia Amos Maganga, akizungumzia tukio hilo, amesema kutokana na hujuma hizo, shirika la Tanesco kwa kipindi cha miezi sita shirika hilo limepata hasara ya shilingi bilioni moja.

Mei 20 mwaka huu Tanesco Mkoa wa Mbeya, lilimkamata Mwantika likimtuhumu kujiunganishia umeme kinyemela na majirani zake na tayari amefikishwa mahakamani.

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top