Bunge la jimbo la jiji la Nairobi
nchini Kenya limepiga kura kuwaondoa makahaba katikati mwa mji mkuu.
Waakilishi katika bunge hilo
walilazimika kupiga kura mara tatu ili kufikia matokeo hayo. Kwa mara mbili
matokeo ya kura yalikuwa sare, lakini baada ya awamu ya tatu kura ya ndio
ikashinda.
Hoja hiyo iliwasilishwa na mwakilishi
Bi Jane Mwasia, ikitaka wakuu wa jimbo kuwaondoa makahaba mara moja kutoka
katikati kwa jiji la Nairobi.
Waakilishi wanaume walipinga hoja
hiyo mara tu ilipowasilishwa lakini mjadala ulipotokota, wengi waliamua kupiga
kura ya ndio wakati wengine wakijizuia.
Mjadala huo nusura uzue makonde
bungeni na kusababisha hisia mseto miongoni mwa waakilishi hao.
Baadhi ya waakilishi hao
walipendekeza kuwa sehemu maalum itengewe makahaba hao baada ya wao kundolewa
katika barabara zilizo katikati mwa jiji.
"sina tatizo na makahaba kwa
sababu wengi wao hawana ajira. Kwa hivyo ni jukumu letu kuwajengea sehemu
ambako wataweza kuendeshea shughuli zao,'' alisema mmoja wa waakilishi hao.
Mwakilishi mwingine, Manoah Mboko
alisema kuwa suluhu kwa makahaba sio kuwaondoa mjini bali ni kuwaoa kwani
sheria ya kuoa zaidi ya mke mmoja ilipitishwa maajuzi. Aliongeza kwamba
makahaba wanachangia pakubwa sana katika uchumi wa mji wa Nairobi.
Mwakilishi mwingine alizua kicheko
aliposema kuwa dunia nzima ni kama soko na hivyo kila mtu aruhusiwe kuuuza
bidhaa zake.
Chanzo BBC SWAHILI








Post a Comment