Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao
Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda usiojulikana licha
ya uamuzi wa mahakama ya leba nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao
kurudi kazini mara moja.
Koti ilikuwa imesema wakuu katika
vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka
yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.
Maandamano mengi yamekuwa
yakulalamikia hali ngumu ya usafiri lakini sasa wafanyikazi wa treni za mijini
ziitwazo Metro ndio waliogoma kutaka nyongeza ya mishahara.
Huku nusu ya vituo vya usafiri
vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.
Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je
hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua
dimba hilo?
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya
mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban
asilimia 9.CHANZO BBC SWAHILI







Post a Comment