![]() |
| Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu |
Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa
miili hiyo ilikuwa chini ya miamba iliopo kwenye mji wa west Bank wa Hebron.
Israel
imepeleka vikosi vyake katika kijiji cha Palestina cha Hal-hul.
Katika
kikao cha dharura cha mawaziri ,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
amesema vijana hao walitekwa na kuuawa katika mauji aliyosema yamefanywa na
wanyama.
Netanyahu
amelilaumu kundi la Wapalestina la Hamas, na akaahidi kulipiza kisasi.
Hamas
imekana kuhusika na mauaji hayo kupitia mshauri rasmi wa rais wa Palestina
Mahmoud Abbas -Abdallah Abdallah
Mwandishi
wa BBC aliyeko mashariki ya kati anasema milio ya mashambulizi ya ndege za
Israeli imesikika kote katika ukanda wa Gaza .
Kulikuwa
na tetesi kuwa Israeli ingeileng maeneo ya Hamas baada ya kikao chake cha
mawaziri cha usalama .
Mji wa
Gaza umesalia kuwa ngome kuu ya Hamas na ofisi zake katika eneo hilo zimekuwa
zikivamiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili na nusu.
vifo
vya karibu wapalestina watano vimeripotiwa na mamia ya wapalestina wamekamatwa.
CHANZO BBC SWAHILI







Post a Comment