Mshambulizi wa Uruguay
na Liverpool ya Uingereza Luiz Suarez sasa amemuomba msamaha mlinzi wa Italia
Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng'ata timu hizo zilipokuwa zicheza
mechi ya mwisho ya makundi huko Brazil.
Suarez aliandika
kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ''baada ya kuketi nyumbani na familia
yangu na kutulia imenijia kuwa tukio la kumng'ata Chellini ni la kusikitisha na
kwamba sitarudia tena .
“ninajutia sana tukio hilo na ninamuomba
msamaha Chellini .ukweli ni kwamba anauguza jereha la kuumwa baada ya kugongana
naye katika mechi hiyo .''
Suarez alimng'ata
mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani
wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.
FIFA imeamuru
asishiriki mechi yeyote ile kwa kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini
ya pauni 65000. (£65,680).
Awali katibu mkuu wa
Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati
akitumikia marufuku hiyo.
Hii si mara ya kwanza
wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani
wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana
na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia
kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez
pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota
huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka
Brazil.









Post a Comment