Na Emanuel Madafa.Mbeya
Hatimaye Timu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmasahuri ya jiji la Mbeya ambayo
inashiriki ligi Tanzania bara leo imetiliana saini katika mkataba mnono kwa
ajili ya kudhamni Clabu hiyo wa
sh.milioni 360 kwa miaka miwili kutoka kampuni ya Binslum ya Jijini Dar es salaam.
Mbeya City
iliyojizolea sifa lukuki kwa mtindo wake wa kuzidindia timu zote zilizocheza
ligi Kuu msimu uliopita imewashawishi wadhamini hao kuwekeza kwa timu hiyo kwa
nia ya kuongeza chachu kwa timu za mikoani zinazocheza Ligi Kuu.
Akizungumza
wakati wa utiani saini wa mkataba huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji leo
asubuhi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Binslum amesema udhamini wao
umelenga kuleta changamoto na hamasa kwa timu za mikoani.
Binslum amesema
kuwa wameamua kuwekeza kwa Timu ya Mbeya City kutokana na namna ambavyo timu
hiyo imeonesha mtindo wa kipekee wa ushawishi kwa soka hapa nchini kinyume na
ilivyozoeleka kwa timu kubwa za Yanga na Simba.
Alisema
kuwa kampuni ya Binslum inaamini itanufaika kwa kutangaza bidhaa zake kupitia
jezi za timu hiyo katika michezo yake kwa msimu wa mwaka 2015-16 na kuwa
wamefikia makubaliano hayo na uongozi wa Mbeya City kutokana na mwitikio mkubwa
wa wapenzi wa soka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba na kampuni hiyo
Meneja Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema kuwa anaamini ufadhili huo utachangia
kuiongezea uwezo timu hiyo katika ligi Kuu msimu ujao wa 2015 na 2016.
Amesema
kuwa mkataba huo utachangia kuongeza kipato cha timu hiyo na kuiwezesha
kujikimu kwa matatizo madogo madogo ambayo anaamini yatatatuliwa kwa ufadhili
huo wa miaka miwili.
Naye Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambaye ndiye mmiliki wa timu hiyo
Dkt. Samwel Lazaro amesema kuwa ufadhili kwa timu za mikoani utachangia klabu
nyingi zisizo na uwezo wa kifedha kushiriki ligi kwa ushindani katika ligi na
kukua kwa soka la Tanzania.
Mwisho.











Post a Comment