![]() |
| Amani Mbwilo Mratibu wa Shindano hilo |
Na Madafa
Emanuel, Mbeya.
Maandalizi ya shindano la kumtafuta Miss Mbeya kwa mwaka 2014 yamefikia katika hatua za mwisho ambapo kesho June 6 mwaka huu mrembo huyo anatarajiwa kupatikana katika viwanja City Pub, ambapo warembo 11 watachuana jukwaani kuwania taji
hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Mbeya Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na kampuni
ya Bomba Fm Radio, Amani Mbilo, alisema mshindi katika kinyang’anyiro hicho
atazawadiwa kiasi cha shilingi 500,000.
Amesema
mshindi wa pili atapata kiasi cha shilingi 300,000, mshindi wa pili 200,000,
huku washiriki wote waliobaki wataambulia kifuta jasho cha fedha kama gharama
ya usafiri wa kufika katika mashindano hayo.
“Washiriki
hawa 11 ni kutoka katika wilaya mbili tu za Mbeya City Centre na Mbeya
Vijijini kutokana na wilaya nyingine kukosa hamasa ya kuendesha
mashindano haya hali iliyosababisha ushiriki uwe wa wilaya mbili tu” alisema
Mbilo.
Mratibu
huyo aliwataja washiriki hao 11 kuwa ni Meryam Cephas, Juliana Gilbert,
Joanitha Tibenderana, Matilda Hillu, Joyce Lameck.
Aliwataja
washiriki wengine kuwa ni Pendo Nelson, Atukuzwe Fabian, Anitha Patrick,
Rhoda Joseph, Felister Godion na Emiliana Abdalah.
Wadhamini
katika shindano hilo ni Tbl kupitia kinywaji cha Reds, Access Computer, Mbeya
Peak Hotel, Kihumbe, Air Tanzania na Dorcus Saloon.
Aidha,
Mbilo alisema katika shindano hilo litasindikizwa na burudani ya bendi ya
muziki wa dansi nchini la Fm Academia kutoka Jijini Dar es salaa na mgeni rasmi
ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.
Mwisho.
![]() |
| Pichani ni warembo waliowahi kushiri shindano hilo picha na maktaba |








Post a Comment