![]() |
Mjumbe wa ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya( NHIF) Ndugu Charles Kajage akitoa salamu za Nhif katika mkutano huo.
|
![]() |
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nhif Kanda ya Nyanda za Juu kusini Dr.Mohamed Kiholile akitoa taarifa kwa viongozi hao juu ya utekelezaji wa Mfuko huo
|
![]() |
| Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Mbeya wakiwa makini kufuatilia agenda za kikao hicho |
![]() |
| Waganga wakuu wa Wilaya na jiji |
![]() |
| Shughuli ya upimaji ukiendleea nje ya Kikao |
![]() |
| Meya wa jiji la Mbeya Atanas Kapunga |
![]() |
| Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mkutano huo . |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro, amesema miongoni mwa changamoto zinazokwamisha hamasa ya
wananchi kujiunga na mifuko ya afya ya jamii ni huduma hafifu zinazotolewa na
watoa huduma katika maeneo husika.
Mkuu huyo wa mkoa
amesema hayo leo jijini mbeya katika ufunguzi wa mkutano wa wadau
wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) Mkoa
wa Mbeya na kujumuisha, wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa
Halmashauri na kufanyika katika ukumbi wa hospitali ya Mkoa kwa lengo la
kujadili utekelezaji wa mfuko huo.
Amesema hadi kufikia
Machi 31 mwaka huu ni kaya 89,841 tu ndizo zilizojiunga na na mfuko wa afya ya
jamii kati ya kaya 635, 037 zilizopo mkoani hapa, ambaya ni sawa na
asilimia 14.15.
Amesema licha umuhimu wa
mfuko huo kwa afya za jamii, mara kadhaa kumeibuka malalamiko yanayoelekezwa
kwa watoa huduma , ambapo wananchi waliojiunga hulalamikia lugha mbaya,
kutopatikana kwa dawa na vifaa tiba.
Amefafanua kuwa changamoto
hiyo kwa ujumla imechangia kwa kiasi kikubwa kuwakatisha tamaa
wananchi, hivyo hata kukwamisha kabisa malengo
yaliyowekwa na serikali kuwa ya kufikia 30 ya watanzania wote kufikia 2015.
Kandoro amesema, kwa
upande wa mradi wa afya ya mama na mtoto muitikio umekuwa ni mkubwa kwani
hadi kufikia sasa zaidi ya familia 70,000 , hivyo kuendelea kunufaika na mradi
huo.
Meneja wa kanda ya
nyanda za juu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF), Dk. Mohamed Kiholile,
alisema utekelezaji wa mfuko huo kwa mkoa wa Mbeya bado si nzuri.
Amesema takwimu
zinaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ndio inaongoza ambapo asilimia
21.42 wakazi wake wamejiunga, huku Halmashauri ya Busokelo ikiwa ya mwisho kwa
uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na mifuko hiyo kwa asilimia 4.15.
Amesema kwa
halmashauri ambazo mratibu wa NHIF na
CHF ni mmoja wateuliwe wawili ili kuongeza ufanisi.
Naye Mjumbe wa bodi ya
wakurugenzi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya, Charles Kajege, aliwataka wakuu
wa wilaya kuwa msitari wa mbele katika kuhamasisha na utekelezaji wa CHF na
upatikanaji huduma bora katika vituo.
mwisho

















Post a Comment