![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi |
Na
EmanuelMadafa,Mbeya
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia Watu
26 kwa kosa la kunywa pombe kabla ya muda.
Watuhumiwa hao walikamatwa June26 mwaka huu majira ya saa 09:30 asubuhi katika Mtaa Wa tukuyu – Tunduma, Wilayani Momba ,M koa wa mbeya katika msako mkali
uliofanyika katika maeneo hayo.
Hata
hivyo teyari watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani cc 26/2014.
Wakati
huo Mkazi wa Nkuyu Ndugu Frank Mwampaja(40) anashikiliwa na jeshi la polisi
mkoa wa mbeya akiwa na pombe kali [viroba] zilizopigwa marufuku na serikali.
Mtuhumiwa alikamatwa June 26 mwaka huu majira ya saa
11:46 asubuhi katika eneo la Itungi-port, kata ya Buloma, wilayani kyela.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na double punch katoni 2 na
boss katoni 1. Taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidzi
mwandamizi wa polisi Ahmed z. Msangi
anatoa wito kwa jamii na wafanyabiashara kwa ujumla kuacha kujihusisha na
uuzaji na usambazaji wa pombe kali zilizopigwa marufuku na serikali kwani ni
kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
Aidha anatoa wito kwa jamii kutoa taarifa za
watu/mtandao wa watu wanaojihusisha na uuzaji na usambazaji pombe kali
zilizopigwa marufuku ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Mwisho







Post a Comment