Na EmanuelMadafa,Mbeya
Uingereza imesema kuwa inafanya mazungumzo na kenya ili kutatua
mzozo kuhusu mafunzo ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo.
Serikali ya Kenya inaaminika kuchelewa kuwaruhusu wanajeshi
zaidi wa Uingereza kuingia nchini humo ili kufanya mazoezi.
Maelfu ya wanajeshi wa Uingereza huzuru nchini kenya kila mwaka
kwa mafunzo ya wiki sita lakini hilo limesitishwa kwa mda baada ya kenya
kuchelewa kutoa ruhusa ya kidiplomasia kwa ndege inayowabeba wanajeshi
wanaotarajiwa kufanya mafunzo hayo.
Hatua hiyo inaonekana kama kulipiza kisasi kwa tahadhari ya
kusafiri humu nchini iliotolewa na serikali ya Uingereza kwa raia wake ambayo
imeathiri pakubwa sekta ya utalii nchini.
Wanajeshi wa Uingereza wamekuwa wakifanya mafunzo nchini kwa
zaidi ya miongo minne lakini makubaliano kati ya mataifa hayo mawili kuhusu
mafunzi hayo yanakamilika mwezi Aprili.
Masineta kutoka upande wa chama tawala nchini kenya wamemtaka
rais Uhuru kenyatta kutotia sahihi mkataba mpya.
Maafisa katika ubalozi wa Uingereza wameiambia BBC kwamba wana
matumaini mgogoro huo utatatuliwa kwa haraka.
Wizara ya maswala ya kigeni nchini kenya hatahivyo inasema kuwa
swala hilo tayari limetatuliwa.CHANZO BBC SWAHILI







Post a Comment