Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro


Na EmanuelMadafa,Mbeya
JUMLA ya Miradi 80 ya Maji inatekekelezwa mkoani mbeya kwa mwaka 2013~14 katika vijiji 112  ambapo kati ya hivyo  miradi 16 imekamilika.
Vijiji hivyo ni pamoja na  Namkukwe Wilayani Chunya Natambalala Wilayani Momba  pamoja na Kyimo Wilayani Rungwe .
Vingine ni Kikuba  Busokelo na Ubaruku Chimala   Simike pamoja na Mbembe ,Masoko. Ikombe ,Maninga  ,lwalanje  na Igale .
Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro imefafanua kuwa  katika miradi hiyo teyari 54 iko katika hatua mbalimbali za  ujenzi na mingine 10 iko katika hatua za mchakato wa Zabuni.
Amesema katika miradi hiyo 80  jumla ya shilingi bilioni 39.4  zinategemewa kutumika  hali ambayo itainua kiwango cha upatikanaji wa  hudumza za maji kwa maeneo ya vijijini na kufikia asilimia 71.8 .
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya mkoa wa mbeya unajumla ya miundombinu ya maji 1,331 pamoja vituo vya kuchotea 5,171 ambapo hadi kufikia mwezi mwaka huu asilimia 56.2 wanapata huduma ya maji.

Mwisho

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top