Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Ndugu Amani Kajuna mwenye miwani akiwa pamoja na kamati ya utekelezaji Uvccm Mkoa wa Mbeya katika Mkutano na Waandishi wa Habari

Muda wa Maswali kwa Waandishi wa Habari


 Na EmanuelMadafa,Mbeya

Baraza la kuu la Umoja  wa Vijana( Uvccm) Mkoa wa Mbeya, linakutana jijini Mbeya   na kujadili mambo kadhaa likiwemo suala la uchaguzi ujao wa serikali za Mitaa unaotalajiwa kufanyika hivi karibuni .

Mbali hilo pia umoja huo upo katika maandalizi  ya mwisho kwa ajili ya kuwasimika makanda 11 wa vijana ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mikakati iliyojiwekea chama kwa kila mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Ndugu Amani Kajuna amesema  uchaguzi wa serikali za mitaa ndio sehemu ya misingi ya siasa kwa chama chochote kile kujipima.

Amebainisha kuwa baraza hilo litatumia kikao hicho   kujadili na kupanga mikakati ili kuona ni jinsi gani watakavyo ibuka na ushindi mkubwa katika chaguzi hizo sanjali na uchaguzi ujao 2015..

Aidha Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa katika kuelekea katika chaguzi za serikali mitaa ndio misingi mikuu ya vyama ifikapo kwenye uchaguzi mkuu  hivyo mikakatia hivyo kama mikakati ya umoja huo itakuwa mizuri chama cha mapinduzi kianuwezo wa kuyarudisha majimbo yote yaliyochukuliwa na upinzani.

Aidha Kajuna amesema kuwa mbali na kujadili suala la chaguzi za serikali za Mitaa pia Baraza hilo litajadili  mstakabali wa Taifa hasa katika harakati za upatikanaji wa Katiba mpya.


Hata hivyo Kajuna ameweka wazi juu ya usimikwaji wa Makamanda  11 ambao unatalajiwa kufanywa julai 6 mwaka huu sherehe ambazo zitafanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya na kuhudhuliwa na  Meya wa Jiji la Ilala Jerry Slaa.


Amesema wao kama  vijana wanapaswa kuwekana sawa hasa kipindi hiki ambacho nchi inatarajia kupata Katiba mpya kwa kuhakikisha wanajipanga na kusimama imara ili kuhakikisha kuwa  ujio huo wa katiba hauthiri nchi kama ilivyotokea maeneo mengine.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top